• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Kumbukumbu za Wachina kuhusu maonesho ya kimataifa kwenye makavazi ya mji wa Shanghai

    (GMT+08:00) 2010-09-23 11:08:25

    Maonesho ya kimataifa ya Shanghai ya mwaka 2010 yanaendelea, makavazi ya mji wa Shanghai yaliandaa maonesho yaitwayo "mafaili ya maonesho ya kimataifa, kumbukumbu za China" katika "jengo la kale la Fayou", ambalo ni jumba la makavazi hayo linalofunguliwa kwa umma. Vitu karibu 100 vyenye thamani kubwa vya maonesho ya kimataifa na picha zaidi ya 200 za kihistoria vinaoneshwa katika maonesho hayo, ili kukumbusha ndoto za Wachina kuhusu maonesho ya kimataifa.

    Mkuu wa makavazi ya mji wa Shanghai Bw. Wu Chen alizungumzia kwa furaha vitu na picha zinazooneshwa kwenye maonesho hayo. Alisema vitu hivyo vyenye thamani kubwa vinavyohusu uhusiano kati ya China na maonesho ya kimataifa toka enzi na dahari ni zawadi iliyotolewa na makavazi ya sehemu mbalimbali nchini China kwa maonesho ya kimataifa ya Shanghai, na kwa watalii wanaotembelea maonesho ya kimataifa. Bw. Wu alisema,

    "Maonesho hayo yameonesha vitu vyenye thamani kubwa kuhusu maonesho ya kimataifa, ambavyo vilichaguliwa kutoka makavazi ya mikoa mbalimbali ya China. Vitu hivyo vinaonesha ndoto za Wachina kuhusu maonesho ya kimataifa, na viko vinaoneshwa katika sehemu tatu ambazo ni China 'kushiriki kwenye maonesho ya kimataifa', 'kuomba kuandaa maonesho ya kimataifa' na 'kuandaa maonesho ya kimataifa'. Baada ya kutembelea maonesho hayo, watazamaji wanaweza kupata uelewa zaidi kuhusu ugumu waliopata mababu zetu kushiriki kwenye maonesho ya kimataifa kwa ajili ya kutafuta njia ya kustawisha taifa letu, na fahari ya China kwa hivi leo kuweza kufanya mazungumzo kwa usawa na nchi mbalimbali duniani na kunufaika na maendeleo yanayopatikana kwa binadamu."

    mwaka 1926

    Kwa mujibu wa kumbukumbu za historia, Wachina walianza kushiriki kwenye maonesho ya kimataifa kuanzia maonesho ya kimataifa ya awamu ya kwanza yaliyofanyika mwaka 1851 huko London Uingereza. Baada ya hapo, serikali za China na makundi yasiyo ya kiserikali yalishiriki kwenye maonesho ya kimataifa kwa njia mbalimbali. Mpaka karne ya 19 njia ya kuinua hadhi ya nchi kupitia kuandaa na kushiriki kwenye maonesho ya kimataifa ilikuwa imekubaliwa na nchi nyingi. Katika kumbukumbu za serikali ya enzi ya Qing, rekodi kuhusu maonesho ya kimataifa zilizidi 1,000. Maonesho hayo pia yalionesha baadhi ya data za enzi hiyo katika sehemu ya "vitu vyenye thamani kubwa vinavyobaki kuhusu maonesho ya kimataifa". Bw. Wu Chen alisema,

    "Maonesho hayo yalionesha barua ya kidiplomasia iliyokabidhiwa mwezi Oktoba mwaka 1870 na balozi wa Austria nchini China kwa ofisi ya waziri mkuu ya serikali ya enzi ya Qing, na barua ya kidiplomasia ya balozi wa Marekani nchini China kwa ofisi ya waziri mkuu wa serikali ya enzi ya Qing mwezi Agosti mwaka 1877, ambayo iliishukuru serikali ya Qing kuyaunga mkono maonesho ya kimataifa ya Philadelphia ya mwaka 1876 na kuitakia China heri na baraka. Maonesho hayo pia yalionesha data kuhusu hali ya serikali ya enzi ya Qing kwa mara ya kwanza kuwaongoza rasmi wafanyabiashara kuhudhuria maonesho ya kimataifa ya St. Louis ya Marekani mwaka 1904."

    Kupitia maonesho ya sehemu hiyo, tunaweza kugundua kuwa ingawa serikali ya enzi ya Qing iliunda idara maalum ya kushughulikia mambo ya nchi za nje, ambayo ilikuwa ofisi ya waziri mkuu, lakini wakati ule forodha ya enzi ya Qing ilifanya kazi kubwa katika kushiriki kwenye maonesho ya kimataifa ya nchi za kigeni. Wafanyakazi wa forodha walishughulikia kazi ya kukusanya vitu vya kuoneshwa kwenye maonesho ya kimataifa.

    Baada ya kutembelea sehemu hiyo ya "vitu vyenye thamani kubwa vinavyobaki kuhusu maonesho ya kimataifa", tunafika katika sehemu ya "kutimiza ndoto ya kuandaa maonesho ya kimataifa". Sehemu hii inaonesha mchakato wa China mpya kutimiza ndoto ya kuandaa maonesho ya kimataifa baada ya kuanzishwa kwake. Bw. Wu Chen alisema katika sehemu hiyo kuna mafaili mengi yanayooneshwa kwa mara ya kwanza, ambayo yanathibitisha kuwa katika miaka ya 50 ya karne iliyopita, China mpya ilikuwa inataka kuandaa maonesho ya kimataifa, na katika miaka ya 80 ya karne iliyopita, mji wa Shanghai ulianza kufanya uchunguzi kuhusu uwezekano wa kuandaa maonesho ya kimataifa. Bw. Wu Alisema,

    "Mafaili yanayotolewa kwa mara ya kwanza na jumba la kuhifadhia mafaili ya serikali kuu yameonesha ripoti iliyotolewa mwaka 1958 naibu waziri wa mambo ya nje wa zamani wa China Bw. Zhang Wentian ya mapendekezo kuhusu serikali ya China kuandaa maonesho makubwa yanayofanana na maonesho ya kimataifa mjini Shanghai katika wakati mwafaka, na maagizo ya hayati waziri mkuu Zhou Enlai. Aidha, data nyingine zinaonesha kuwa mwaka 1985 wakati mji wa Tsukuba wa Japan ulipoandaa maonesho ya kimataifa, taasisi ya sayansi ya jamii ya Shanghai iliualika 'ujumbe wa uchunguzi kuhusu uwezekano wa Shanghai kuandaa maonesho ya kimataifa' kutembelea China, ambapo Shanghai ilitoa wazo la kuomba kuandaa maonesho ya kimataifa, na kwa mara ya kwanza ilitoa wazo la kuunganisha maandalizi ya maonesho ya kimataifa na uendelezaji wa sehemu ya Pudong."

    mwaka 1851

     

    Tarehe 3 Desemba mwaka 2002 mji wa Shanghai China, ulichaguliwa kuwa mwenyeji wa maonesho ya kimataifa ya mwaka 2010, kwa hiyo China imekuwa nchi ya kwanza inayoendelea kupewa nafasi ya kuandaa maonesho ya kimataifa.

    Maonesho ya "mafaili ya maonesho ya kimataifa, kumbukumbu za China" yamewavutia watalii wengi toka yalipofunguliwa mwishoni mwa mwezi Aprili. Katika likizo ya majira ya joto, maonesho hayo pia yaliwasaidia wanafunzi wa sehemu mbalimbali kuelewa kwa undani zaidi juhudi za China kutaka kuandaa maonesho ya kimataifa.

    Inafahamika kuwa ili watalii wengi zaidi waweze kuelewa mchakato wa China kutimiza ndoto yake ya kuandaa maonesho ya kimataifa, maonesho hayo yataendelea kufanyika hadi mwishoni mwa mwaka huu.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako