• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Kujionea utamaduni wa bia kwenye mgahawa wa kijerumani

    (GMT+08:00) 2010-09-27 20:14:18

    Mgahawa wa jumba la maonesho la Ujerumani lililoko kwenye eneo la maonesho ya kimataifa ya Shanghai ni moja kati ya migahawa michache mikubwa iliyoko kwenye maonesho ya kimataifa ya Shanghai. Mgahawa huo unapendeza na unavutia watalii waliotoka sehemu mbalimbali za dunia kwa chakula halisi cha Ujerumani. Katika siku za joto, kupata bia baridi ya Ujerumani bila shaka ni chaguo la watalii wengi.

    Wajerumani wanapenda sana kunywa bia, nchini humo kuna makundi zaidi ya 20 na aina zaidi ya 1,500 za bia, mauzo ya bia zake yanachukua nafasi ya kwanza duniani. Ili kuwapatia bia halisi za Ujerumani watazamaji wanaotembelea maonesho ya kimataifa, kampuni maalumu ya huduma za chakula ya Angerer na Obermayr, ambayo inashughulikia uendeshaji wa migahawa ya Ujerumani, ilileta zana za mgahawa na mali-ghafi ya bia kutoka Ujerumani. Bia halisi ya Ujerumaji inapendwa na watu wengi, hadi hivi sasa, mgahawa huo wa Ujerumani umeuza bia karibu lita laki moja, kati ya bia hizo, ile bia nyeusi inapendwa zaidi na watu. Meneja mkuu wa mgahawa huu wa Ujerumani, ambaye ni kiongozi wa kampuni ya huduma ya chakula ya Angerer na Obermayr Bwana Gerhard Obermayr anasema,

    "Kati ya bia zote zilizouzwa, asilimia 60% ni bia nyeusi, asilimia 30% ni bia za ngano, na asilimia nyingine 10% ni bia za lager. Bia nyeusi zinapendwa na wachina wengi, kwa kuwa bia hiyo licha ya kuwa na ladha chungu, ina ladha tamu kidogo, ambayo ni ladha wanayoipenda wachina. Hasa katika majira ya joto, watu wanaipenda zaidi."

    Hasa wakati wa adhuhuri na jioni wakati watu wanapokula chakula, viti vyote kwenye mkahawa huo wa Ujerumani vilijaa watu. Karibu kila mlaji aliagiza glasi moja ya bia. Bw Gerhard Obermayr alisema, mwaka 1516 Ujerumani ilibuni kanuni za utengenezaji wa bia, ambazo zinafuatwa kwa makini na watengenezaji wa bia wa nchi hiyo, kwa hiyo hali ya bia za nchi hiyo inadumishwa hadi hivi sasa. Kama anavyosema ,

    "Kanuni zilizotolewa na Ujerumani kuhusu utengenezaji wa bia, zinaeleza kuwa bia zinatengenezwa kwa maji, punje za shairi zinazoanza kuchipuka na hops peke yake. Lakini katika baadhi ya nchi, watengenezaji wa bia huchanganya mchele na unga."

    Ingawa mali-ghafi zinazotumika katika utengenezaji wa bia ni aina chache sana, lakini wajerumani wanaweza kuzitumia kutengeneza bia zenye ladha, rangi na viwango tofauti vya kilevi. Bw Gerhard Obermayr alichukulia mfano wa kutengeneza bia nyeusi akisema, kutengeneza bia ya aina hiyo kunahitaji maji magumu (Water Hardness), na hali ya maji ya Munich, Nchini Ujerumani inakidhi masharti hayo. Pili, ni kuchagua shayiri nzuri, na kuzitia katika maji mpaka zianze kuchipuka, halafu zikaushwe kwa joto la kiwango kinachofaa. Kazi ya kukausha shayiri zilizochipuka ni kazi muhimu sana. Alisema,

    "Wakati wa kukausha shairi zinazoanza kuchipuka, joto tofauti litasababisha bia kuwa na rangi tofauti na yenye kiwango tofauti cha kilevi. Ikiwa wakati wa kukausha shairi kutakuwa na joto kubwa sana, shairi inabadilika kuwa na rangi nyeusi, shairi ikichanganywa pamoja na maji na vitu vingine, maji yanabadilika kuwa na rangi nyeusi. Kwa kawaida joto la nyuzi 80 linafaa kwa utengenezaji wa bia, lakini kutengeneza bia nyeusi kunahitaji joto la nyuzi 100. Tofauti ya joto ni nyuzi zaidi ya 20, joto linafanya shairi zilizochipuka kuwa na rangi nyeusi, hivyo rangi ya bia pia inakuwa nyeusi. Kwa sababu wakati wa kukausha shairi zilizochipuka kwa joto kubwa, kwa hiyo ladha ya bia nyeusi ni tamu zaidi kuliko ile ya kawaida. Nchini Ujerumani, bia nyeusi zilizotengenezwa na viwanda mbalimbali, utamu wake pia ni tofauti. Hii ndiyo sababu ya kuweko bia nyeusi za aina mbalimbali nchini Ujerumani."

    Kuweko aina nyingi za bia, inawapa watu nafasi kubwa ya kuchagua bia wanazopenda, kwa hiyo wajerumani ni watu wanaopenda sana kunywa bia. Kila siku wajerumani wanakunywa bia toka asubuhi hadi usiku, kwa wajerumani bia si aina moja ya kinywaji, bali ni sehemu moja muhimu ya maisha yao. Inasemekana, katika viwanda vya nchini Ujerumani bia ni kama vinywaji vya aina nyingine, ambavyo vinawekwa katika jokofu, wafanyakazi wanaruhusiwa kunywa wakati wowote. Kwa hiyo, wajerumani wana uwezo mkubwa wa kunywa bia, takwimu zinaonesha, kila mkazi wa jimbo la Bavaria anakunywa wastani wa lita 235.7 kwa mwaka. Bila shaka, bia haitumiwi na wanaume peke yao, hata wanawake wana uwezo mkubwa wa kunywa bia. Msichana Mareen Hoeppner anabainisha,

    " Tofauti na wachina ni kuwa, katika majira ya joto sisi tunapenda kujiburudisha katika mwangaza wa jua huku tukinywa bia, wala siyo kunywa bia katika nyumba zenye viyoyozi(air conditioner). Tena, sisi hatuna glasi ya lita 1, glasi zetu tunazotumia kunywa bia ni za lita 3.5. Wajerumani wote wanapenda kukaa sehemu za wazi, hasa wakati wa majira ya baridi, tunapenda vivyo hivyo. Ni kweli kabisa wajerumani wanaburudika kutokana na furaha zinazosababishwa na bia."

    "Sehemu za wazi"(open space) alizotaja dada Mareen Hoeppner ni "bustani ya bia", ambayo ni mahali pa kunywa bia kwa wajerumani katika majira ya joto. "Bustani ya bia" ni mahali pa wazi kama baa: panaweza kuwa chini ya mti mkubwa kwenye ua la nyuma la mgahawa, au panaweza kuwa ni kiwanja chenye majani pembeni mwa kiwanda cha bia, hata chini ya miavuli mikubwa kando kando mwa barabara. "Bustani ya bia" inaweza kuwa kubwa au ndogo. Ile kubwa inaweza kuchukua watu 2,000 hadi 4,000.

    Mgahawa wa jumba la maonesho la Ujerumani kwenye eneo la maonesho ya kimataifa ya Shanghai, una "bustani ya bia" kama hiyo: huko zimewekwa meza na viti vya rangi nyeupe, wahudumu wa kijerumani waliovaa nguo nyeupe na sketi nyeusi wakiwahudumia wateja, mtu akiwa katikati yao, anajisikia kama yuko kwenye mtaa wa Munich nchini Ujerumani.

    Katika "bustani ya bia" unaweza kujiburudisha peke yako, vilevile unaweza kukaa pamoja na marafiki kadhaa, hivyo mnaweza kunywa bia huku mkiongea.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako