• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Barua za wasikilizaji

    (GMT+08:00) 2010-09-28 19:23:39

    Msikilizaji wetu Anifa A. Byemelwa wa Ukonga DSM Tanzania, ametuletea barua pepe akisema nawapongeza CRI kwa kazi ngumu ya kuwatafuta washindi wa chemsha bongo ya mahusiano ya kibalozi kati ya China na Tanzania. Wasikilizaji tumekutana na kufahamiana kwa sura. Pia tumezifurahia zawadi nzuri mlizotuandalia. Tudumishe urafiki ili tuelimike zaidi. Nawatakia kazi njema.

    Barua pepe nyingine inatoka kwa msikilizaji wetu epafra Stanley wa Dar es salaam Tanzania, anasema ilikuwa ni siku ya furaha kwetu sisi wasikilizaji wenu ambao tuliweza kukutana uso kwa macho na wasikilizaji ambao tumekuwa tukiwasiliana nao kupitia CRI, ambapo imetuwezesha kufahamiana, kwa kweli ilikuwa ni siku ya furaha sana sana. tukiwa na furaha sana kupokea tuzo hizo napenda kuwashukuru sana uongozi mzima wa REDIO CHINA KIMATAIFA kwa kutupatia tuzo hizo. Udumu urafiki kati yetu. Asante sana.

    Bwana Lenusi kingalu wa S.L.P 24 Kihonda Morogoro Tanzania, anasema mkurugenzi, meneja, wahariri, kitengo cha maandalizi ya chemsha bongo na wafanyakazi wote, nawashukuru kwa kunichagua hata kunikutanisha na wasikilizaji wa CRI nchini Tanzania, nawashukuruni kwa zawadi nzuri ya runinga, mimi na familia yangu tunasema asante sana.

    Nimejifunza kitu kingine kuwa CRI si tu mnasonga mbele zaidi katika mpango huu, CRI inawajali wasikilizaji na inaonesha namna inavyotuthamini watanzania, mbali na urafiki uliopo lakini kitendo cha kutoa zawaidi za kuwaalika washindi China kwa gharama zenu. Ni wazi kuwa kweli mna nia ya kutufanya watanzania tujifunze mambo mengi zaidi toka China. Tuzo za cherehani, hii ni moja ya kutufanya tujiajiri na kuondokana na umasikini, runinga, hii ni sehemu mojawapo ya kutufanya kutazama habari mbalimbali ili tuweze kujifunza mengi hususani katika ulimwengu huu wa sayansi na teknolojia.

    Nawashauri watu wengine ambao hawasikilizi Redio China Kimataifa, waanze kuisikiliza sasa kwa maendeleo ya jamii na uchumi wa taifa kwa ujumla. Nimegundua kuwa China haijipatii tu maendeleo yake tu, bali na mataifa mengine pia hii nimejionea katika sherehe ya utoaji tuzo ubalozini Dar es Saalam nami nikiwa mmoja wao. Tuendelee kuisikiliza CRI daima.

    Msikilizaji wetu Damas Bundala wa Dar es Salaam Tanzania anasema ndugu watangazaji wapendwa, napenda kuwashukuru kwa zawadi mliyonipatia kama mmoja wa washindi wa nafasi ya kwanza katika chemsha bongo ya miaka 45 ya uhusiano kati ya China na Tanzania, kwenye sherehe ya utoaji tuzo iliyofanyika tarehe 22 Septemba 2010, katika ubalozi wa China nchini Tanzania.

    Niliweza kuhudhuria sherehe hiyo na nilifurahi sana, kwanza kukutana na wasikilizaji wengine mbalimbali wa CRI ambao sikuwahi kuwaona ana kwa ana isipokuwa kwenye kipindi cha salamu tu. Pia nilifurahia sana shughuli mbalimbali zilizoendeshwa mahali pale.

    Napenda pia kuwapongeza washindi wote wa chemsha bongo hiyo, na kuwatia moyo wale wote ambao hawakuweza kushinda nafasi yoyote kwamba wasikate tamaa, waendelee kushiriki na siku moja wataweza kushinda. Mungu awabariki sana, wafanyakazi wote wa CRI.

    Tunawashukuru sana wasikilizaji wetu wote mlioshiriki kwenye sherehe ya kutoa tuzo ya chemsha bongo ya maadhimisho ya miaka 45 ya uhusiano wa kibalozi kati ya China na Tanzania, tunawasihi muendelee kusiokiliza vipindi vyetu zaidi, ahsanteni sana.

    Msikilizaji wetu Stephen Magoye Kumalija wa S.L.P 1067 Shinyanga Tanzania, anasema napenda kutumia wasaa huu nikitumai kuwa nyote hamjambo sana marafiki zetu waheshimiwa wafanyakazi wa idhaa ya Kiswahili ya redio China Kimataifa huko Beijing. Mimi huku niko salama wa salimini nikiendelea kufuatilia matangazo ya redio China Kimataifa pamoja na kuiandikia barua.

    Awali ya yote napenda kuwashukuru watangazaji ambao ni shupavu na imara wa redio China kimataifa mama Chen na Pili Mwinyi katika kipindi cha sanduku la barua cha tarehe 2 Machi mwaka 2010, walipokuwa wakisoma barua pamoja na kujibu barua hizo za wasikilizaji wenzangu wa CRI mmoja kutoka Tanzania na mwingine kutokja Kenya, ambapo maswali ya wasikilizaji yalikuwa yakilenga majina ya washindi wa chemsha bongo tunazozizafanya sisi wasikilizaji wa CRI za mwaka 2008 na 2009.

    Ambapo watangazaji wangu mabibi Chen na Pili Mwinyi wametutoa hofu kuwa tuwe na subira kutangazwa kwa majina ya washindi pamoja na kutuma zawadi zao, kuhusu chemsha bongo ya maadhimisho ya miaka 45 ya uhusiano wa kibalozi kati ya China na Tanzania, hivyo basi ndugu wa CRI sina budi kuvuta subira mpaka wakati mtakapotangaza hapo baadaye kuhusu majina ya wasikilizaji washindi wa chemsha ya mwaka jana, kwani ndugu zangu watumishi wa CRI kufika muda mrefu kama huu wengi wetu tulishakata tama kuwa kumbe marafiki zetu wachina ni waongo, kumbe sio hivyo. Kwahiyo nasubiri majibu hayo kwa hamu kubwa, ahsanteni sana marafiki zangu.

    Nasi tunakushukuru sana msikilizaji wetu Stephen Magoye Kumalija. Tunatumai kuwa sasa utashusha pumzi wewe na wasikilizaji wetu wote walioshiriki kwenye chemsha bongo ya maadhimisho ya miaka 45 ya uhusiano wa kibalozi kati ya China na Tanzania kwani majina ya washindi tayari tumeshatangaza na wiki iliyopita sherehe ya kutoa tuzo imefanyika katika ubalozi wa China nchini Tanzania na tunapenda kuchukua fursa hii kuwashukuru na kuwapongeza wale wote waliobahatika kushinda nafasi mbalimbali. Mwisho tunawaomba muendelee kushiriki zaidi kwenye chemsha bongo tunazozitoa. Ahsanteni.

    Msikilizaji wetu Mchana J Mchana wa S.L.P 1878 Morogoro Tanzania, anasema propaganda zinazoenezwa kuhusu pikipiki na simu za China zinazoletwa nchini Tanzania na wafanyabiashara ni muhimu kuzielezea. Kwakweli mwanzoni propaganda hizo za wafanya biashara na nchi zenye chuki na biashara za China kuwa pikipiki za China ni feki, na Afrika nzima ilijua vitu vyote vya China ni feki, lakini kwasasa watu wengi wamefahamu kuwa maneno hayo yote ni propaganda tu, na China ni mkombozi wetu.

    Pikipiki za China zimewafanya watanzania kupata ajira, simu nazo ndio zina soko kwani zinakidhi mahitaji ya mtu mwenye kipato cha chini, hongera China kwa kutujali tulio na kipato kidogo.

    Ahsante sana bwana Mchana J Mchana kwa maoni yako, sisi tunapenda kuungana nawe, kwani si sahihi kabisa kusema china inatengeneza na kupeleka bidhaa feki katika nchi za Afrika, ukweli ni kwamba hizo ni propaganda za kutaka kuuwa soko la China katika nchi za Afrika na ulimwenguni, lakini tunafurahi kuona kuwa watu sasa wamefahamu undani wa maneno hayo kuwa hayana ukweli wowote. Mwisho tunapenda kutoa mapendekezo kwa wafanya biashara wote wajaribu kuwa makini wakati wanaponunua bidhaa kwaajili ya kuwauzia wananchi wa kawaida kwani kutokuwa makini ndio kunasababisha matatizo yote hayo.

    Sasa ni barua kutoka kwa Bwana Arnold muhatia wa S.L.P 370-50200 Bungoma Kenya, anasema mimi ni shabiki mkubwa wa Redio China Kimataifa na ningependa kuwapongeza kwa kazi yenu nzuri ya utangazaji, kwa kweli huduma mnayotupa ni ya kufana. Mbali na haya ningependa kuwashukuru kwa taarifa zenu za uwazi na zisizoegemea upande wowote. Nashukuru sana na Mungu awabariki.

    Msikilizaji wetu mwingine ni Nelson Charles Ombogo wa S.L.P 38-50301 Bunyore Kenya, naye anasema kuwa natoa shukurani nyingi kwa huduma muhimu mnayotupatia sisi mashabiki mbalimbali, tunawapata kwa njia safi. Ningependa kusema kuwa ikiwezekana murudie mtindo wa zamani kwa upande wa salamu kuanzia saa 11 jioni kwa saa za hapa Kenya.

    Tunawashukuru sana wasikilizaji wetu Arnold muhatia na Nelson Charles Ombogo kwa barua fupi, hata sisi pia tunafurahi sana tukiona wasikilizaji wetu wanaridhika na matangazo yetu, kubwa ni kukuombeni muendelee kutuma barua na kutoa maoni yenu kuhusu mambo mbalimbali. Ahsanteni sana.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako