Tume maalum ya kulinda amani ya Umoja wa Mataifa nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo tarehe 7 ilitoa maofisa na askari 218 wa kikosi cha 11 cha kulinda amani cha China nishani ya Umoja wa Mataifa, ili kuwasifu kwa mchango wao wa kusukuma mbele mchakato wa amani nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo.
Hafla ya kutoa nishani ilifanyika kwenye eneo la jukumu mjini Bukavu, mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo. Amrijeshi mkuu wa kikosi cha kulinda amani cha tume maalum Bw.Purakash alisema kikosi cha kulinda amani cha China kimeboresha miundo mbinu ya barabara na hali ya matibabu kwenye eneo la Bukavu, vitendo na nidhamu yao vilevile vimekuwa mfano wa kuigwa kwa tume maalum.
Ofisa mtawala wa tume maalum kwenye eneo la Kusini-Bukavu Bw. Saina vilevile aliwashukuru wanajeshi wa China kwa kutoa mchango mkubwa katika operesheni ya kulinda amani ya Umoja wa Mataifa na kwa ajili ya wananchi wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo.
© China Radio International.CRI. All Rights Reserved. 16A Shijingshan Road, Beijing, China. 100040 |