• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Michezo ya jadi ya makabila madogo madogo mkoani Xinjiang  

    (GMT+08:00) 2010-10-14 15:50:52

    Kwenye mkoa wa Xinjiang kuna makabila mbalimbali, na michezo ya jadi ya huko pia ni ya aina mbalibali na yenye umaalumu wa kipekee. Michezo ya jadi ya makabila madogo madogo ya Xinjiang yaliyofanyika hivi karibuni huko Hami yamewavutia wachezaji karibu elfu moja kushiriki na kufanya maonesho.

    Katika siku ya ufunguzi wa Michezo ya 7 ya jadi ya makabila madogo madogo ulifanyika, kituo cha michezo cha Hami kinachoweza kuchukua watu elfu 10 kilijaa watazamaji wenye furaha kubwa.

    Mkazi wa huko Sha Fei alifurahi sana baada ya kutazama ufunguzi huo, anasema,

    "Ufunguzi huo ni mzuri. Mpangilio wa jukwaa unaochanganya mbinu mbalimbali za uoneshaji unawavutia sana macho."

    Mkoa wa Xinjiang ni sehemu yenye makabila mbalimbali, ambapo watu wa makabila mbalimbali yanaishi pamoja kwa maskilizano, na pia utamaduni wa mkoa huo ni wa aina mbalimbali. Michezo ya jadi ya mkoa huo ni kuchanganya ushindani, maonesho, dansi na burudani, na inaburudisha sana watu. Makabila madogo madogo mengi yanayoishi katika mkoa wa Xinjiang yanaishi kwa kutegemea kufuga wanyama, na chanzo za michezo ya makabila hayo ni kutokana na maisha yao ya ufugaji, ndiyo maana, michezo ya mbio za ushindani wa farasi, kunyang'anya mbuzi kwa kupanda farasi na kulenga shabaha kwa kupanda farasi ni michezo ya jadi inayokaribishwa zaidi na watu.

    Mbio za ushindani kwa kutumia boriti za mianzi ni mchezo mpya unaoongezwa kwenye michezo hiyo ya makabila madogo madogo. Huu ni mchezo wa jadi unaoenea katika sehemu yenye makabila madogo madogo zilizoko kusini na kusini-magharibi nchini China. Mwamuzi wa mchezo huo Bw. Yin Jiankang anasema,

    "Watu wa kabila la Tujia wakienda nje kutembelea wenzao wakati wa mvua, huwa wanatembea kwa kufunga boriti za mianzi kwenye miguu yao, na baada ya kufika nyumba wanayoitembelea, watashuka kutoka boriti ya mwanzi na kuingia nyumbani, ili kuepusha matope yasiletwe nyumbani."

    Mbio za ushindani kwa kufunga boriti za mianzi ni mchezo rasmi wa ushindani kwenye Michezo ya jadi ya makabila madogo madogo ya China, lakini hii ni mara ya kwanza kwa watazamaji wengi wa Xinjiang kuyatazama mashindano hayo. Mtazamaji Cao Chunfang alisema,

    "Sijayaona mashindano hapo awali, naona furahi sana kwa kupata fursa hiyo ya kuyaona."

    Kulenga shabaha kwa mishale ni mchezo unaofurahishwa sana kwenye Michezo ya makabila madogo madogo. Safari hii umewashirikisha wachezaji 48 wenye uwezo mkubwa kutoka sehemu 10 mkoani Xinjiang. Mwamuzi mkuu wa mchezo huo Bw. Jing Junyi anasema,

    "Michezo hiyo ya wanaume ni pamoja na ya mita 70, mita 90, mita 40 na mita 30, na kwa wanawake ni ya mita 70, mita 60, mita 50 na mita 30. Inatakiwa kulenga mishale 36 katika kila mchezo, na kwa jumla inatakiwa kulenga mishale 144 katika michezo yote."

    Mchezo wa kulenga shabaha kwa mishale ni moja kati ya michezo ya kale kwa makabla ya wa Waxibo, Wauighur na Wamongolia. Baada ya China mpya ianzishwe, mchezo huo umewekwa kwenye michezo rasmi, na upinde na mishale pia zimetengenezwa kuwa za kisasa. Bw. Jing Junyi alisema, umuhimu mkubwa kwa wachezaji ni kujituliza. Anasema,

    "Wachezaji wanaochaguliwa kuchezea mchezo huo wanatakiwa kuwa na tabia yenye utulivu. Aidha wanatakiwa kuwa na nguvu kubwa ya mikono, na kudumisha kiwango chao cha ustadi wakati wa mashindano."

    Kunyang'anya mbuzi kwa kupanda farasi ni mchezo wenye ushindani mkubwa sana. Huu ni mchezo unaokaribishwa sana na makabila ya Wakazak, Wakirgiz na Watajik. Kwenye uwanja wa michezo, makundi mawili yatashindana kunyang'anya mbuzi, na mtu atakayepata mbuzi atafanya juhudi za kufika kituo cha mwisho chini ya ulinzi wa wenzao, na kundi lenye mtu atakayefika kituo cha kwanza huku akichukua mbuzi litashinda.

    Mtazamaji Ma Yan anaona kuwa, huu ni ushindani kati ya washujaa wa Wakazak, si kama tu unahitaji washiriki wenye nguvu kubwa, pia unadai umoja na mshikamano ndani ya makundi. Anasema,

    "Kama Methali moja ya kabila la Wakazak inavyosema: 'mchezo wa mweleka kwaonesha nguvu ya watuna mchezo wa kunyang'anya mbuzi kwaonesha ushupavu wa watu.' Mchezo wa kunyang'anya mbuzi si kama tu unawaburudisha watu, pia unaonesha ushupavu na ushujaa wa watu walioshiriki kwenye mchezo huo."

    Katika Michezo ya 7 ya jadi ya makabila madogo madogo ya Xinjiang, michezo mingine kama vile mapambano ya mbuzi, mbwa na jogoo pia inawafurahisha sana watu. "Wachezaji" hao wanaoundwa na wanyama wanashindana katika uwanja wa michezo. Michezo hiyo inakaribishwa sana katika vijiji venye eneo kubwa mkoani Xinjiang, hususan wakati wa sikukuu. Mtazamaji Lu Xiuchen anasema,

    "Hii ni michezo mikubwa kwa sisi wakazi wa Xinjiang, na inaimarisha mawasiliano kati ya makabila mbalimbali. Nafurahi sana kupata fursa hii kuiona."

    Kulikuwa na michezo mitano tu wakati michezo hiyo ya kwanza ilipofanyika mwezi Septemba mwaka 1985, na katika michezo hiyo ya saba, kumekuwa na michezo mikubwa 12, na michezo midogo mipya 25. Maendeleo ya michezo hiyo yameonesha kihalisi maendeleo yenye masikiliano ya makabila madogo madogo katika mkoa wa Xinjiang.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako