• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Barua za wasikilizaji

    (GMT+08:00) 2010-11-09 19:25:32

    Msikilizaji wetu Mbarouk Msabah Mbarouk wa S.L.P 52483 Dubai, anasema kwanza kabisa ningependa kukujulisheni ya kwamba nimewasili hapa mjini Dubai salama usalimini, baada ya kumaliza ziara yangu hapo nchini China nikiwa miongoni mwa ujumbe wa watu watano, ambao ni washindi wa Shindano la kuadhimisha miaka 45 ya Uhusiano wa kibalozi kati ya Jamhuri ya Watu wa China na Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

    Pili ningependa kutoa shukrani zangu za dhati kwa uongozi wote wa Radio China Kimataifa pamoja na wafanyakazi wake wote, kwa mapokezi mazuri yaliyojaa upendo na ukarimu uliooneshwa kwetu mimi na washindi wenzangu wanne tulipowasili mjini Beijing tarehe 18 mwezi Oktoba mwaka huu kwa ajili ya ziara ya siku kumi. Pia ningeushukuru sana Ubalozi wa Jamhuri ya Watu wa China uliopo Mjini Dar -Es -Salaam Tanzania, kutokana na mchango wake mkubwa wa kugharamia safari yetu hiyo ya kihistoria.

    Mimi binafsi nikiwa kama msikilizaji wa Idhaa ya Kiswahili ya Radio China Kimataifa kwa zaidi ya miaka 20, nimeweza kutimiza ndoto yangu ya muda mrefu ya kupata nafasi ya kuitembelea Jamhuri ya Watu wa China, ili kujionea mwenyewe kwa macho yangu Ustaarabu mkubwa na wa muda mrefu wa Wachina pamoja na kujionea binafsi maisha ya kila siku ya Wachina chini ya mila, desturi na tamaduni za Kijadi za China, pamoja na kushuhudia Maendeleo makubwa ya kiuchumi na kiteknolojiya, ambayo yameweza kufikiwa nchini China hadi sasa.

    Kutokana na mpangilio mzuri ulioandaliwa na Idhaa ya Kiswahili ya Radio China Kimatifa kwenye ziara yetu hiyo, tuliweza kupata nafasi mbali mbali za kutembelea maeneo ya Kihistoria kama vile Uwanja wa Tiananmen pamoja na Kasri ya Kifalme, pia mitaa ya kale mjini Beijing, Bustani mbali mbali za kuvutia kama vile Kasri ya Kifalme ya majira ya Joto, Makumbusho na Maktaba Kuu ya Kitaifa ya China bila kusahau eneo muhimu sana katika historia ya China yaani Ukuta Mkuu , ambao mimi binafsi niliweza kutimiza ahadi yangu ya kuupanda ukuta huo hadi kileleni !!! jambo ambalo sitaweza kulisahau kamwe katika maisha yangu yote.


    1 2
    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako