• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Maisha ya wafanyabiashara kutoka Taiwan mjini Kunshan

    (GMT+08:00) 2010-11-11 15:29:45

    Baada ya kiwanda cha nguo cha Shunchang, ambacho ni kiwanda cha kwanza kilichowekezwa na mfanyabiashara kutoka Taiwan kujengwa huko Kunshan mkoani Jiangsu mwaka 1990, mpaka sasa viwanda vilivyowekezwa na wafanyabiashara kutoka Taiwan vinavyojengwa mjini Kunshan vimezidi 3,700, na thamani ya uwekezaji kutoka kwa wafanyabiashara wa Taiwan inakaribia dola za kimarekani bilioni 45. Baada ya kufanya juhudi kwa miaka 20, hivi sasa watu laki 1 kutoka Taiwan wamenunua nyumba na kuishi huko Kunshan. Wanashiriki kwenye shughuli mbalimbali za utamaduni, elimu, matibabu na hisani, na wamekuwa watu wanaohimiza mawasiliano ya kiutamaduni kati ya China bara na Taiwan.

    Ukitembea katika barabara mjini Kunshan, popote pale utaweza kuona vitu vya Taiwan, hali ambayo inaufanya ujisikie kama uko Taiwan, na wafanyabiashara kutoka Taiwan na jamaa zao wanaoishi hapa wanaupenda mji huo Kunshan.

    Bibi Chen Limei ni mkuu wa Jumuiya ya hisani ya wanawake iliyo chini ya shirikisho la wafanyabiashara kutoka Taiwan. Mwaka 2002 kiwanda cha bibi Chen Limei kilihamishiwa huko Kunshan kutoka Dongguan mkoani Guangdong, hivyo akaanza maisha yake mjini Kunshan. Lakini mwanzoni hakuzoea hali ya huko, alisema,

    "Mwanzoni sikuzoea kabisa kwa sababu washirika wangu wa zamani walikuwa Taiwan. Bado nakumbuka kuwa kitu kilichonishinda mwanzo ni chakula kilichopikwa hapa, kwani wanaweka sukari kwenye mboga waliopika."

    Kadiri wafanyabiashara wengi kutoka Taiwan wanavyofanya biashara huko Kunshan, ndivyo tatizo la bibi Chen Limei linavyozidi kuondolewa. Migahawa ya chai, kahawa pamoja na vitafunwa vyenye asili ya Taiwan vinaonekana hapa na pale huko Kunshan. Mgahawa wa Riyuetan ni mmojawapo.


    1 2
    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako