• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Bibi Liu Zhangzhu, kiongozi wa ujumbe wa michezo wa Hongkong China kwenye Michezo ya Asia ya Guangzhou

    (GMT+08:00) 2010-11-25 18:08:34

    Mkoa wa utawala maalum wa Hongkong unasifiwa kuwa ni "lulu ya mashariki". Katika mkoa huo michezo kutoka nchi za nje kama vile judo, kareti, biliadi, mashua zenye matanga, skwoshi, mchezo wa ustadi wa kutembea wa farasi, mpira wa miguu na mafute inakaribishwa sana. Kwenye Michezo ya 16 ya Asia ya Guangzhou, mkuu wa ujumbe wa Hongkong China bibi Liu Zhangzhu alimfahamisha mwandishi wetu wa habari maendeleo ya michezo mkoani Hongkong.

    Bibi Liu ni mkuu mwanamke pekee wa ujumbe wa michezo, pia ni mkuu mwanamke pekee wa "Mahakama ya mwanzo", alisema,

    "'Mahakama ya mwanzo' ilianzia wakati Hongkong ilipokuwa koloni la Uingereza, hakimu wa mahakama hiyo anaweza kuwa jaji mdogo, pia anaweza kufungisha ndoa. Baada ya kurudi China, serikali ya Hongkong imeendelea kubakiza heshima ya Mahakama ya mwanzo. Lakini ukitaka kupata heshima hiyo, lazima ufanye kazi nyingi za jamii, kwa mfano tunatoa mchango kwa jamii katika mambo ya michezo, hivyo serikali ya Hongkong inatupa heshima hiyo."

    Bibi Liu Zhangzhu alimwambia mwandishi wetu wa habari kuwa alianza kushughulikia mambo ya michezo wakati alipokuwa mwanafunzi wa shule ya sekondari. Baada ya kustaafu amekuwa mwenyekiti wa shirikisho kuu la mafute. Alisema furaha na masikitiko yote yanatokana na mambo ya michezo, ingawa karibu muda wake wote unatumiwa kushughulikia mambo ya michezo, lakini haoni majuto, na bado anaendelea kufanya juhudi ili kuhimiza maendeleo ya michezo mkoani Hongkong. Safari hii Hongkong imetuma ujumbe wenye wachezaji wengi zaidi kushiriki kwenye Michezo ya Asia ya Guangzhou, na Bw. Huo Qigang kwa mara ya kwanza ameongoza ujumbe wa michezo wa Hongkong akiwa naibu mkuu wa ujumbe huo. Bibi Liu Zhangzhu alijulisha kuwa,

    "Kama baba yake, Bw. Huo Qigang anapenda michezo, hivyo baba yake anataka kumwandaa kushughulikia mambo ya michezo ya kimataifa. Mimi pamoja na Bw. Guo Zhiliang, ambaye ni naibu mkuu wa shirikisho la michezo la Hongkong pamoja na kamati ya michezo ya Olimpiki, tumekuwa wakuu wa ujumbe wa michezo wa Hongkong kwa miaka mingi, na sote tunaona kuwa ni lazima kumwandaa kijana kuendelea na kazi zetu, ili awe na fursa ya kujionesha."

    Bibi Liu Zhangzhu alisema kuanzia utotoni ameishi katika mazingira ya michezo. Alikumbuka kuwa baba yake ni hodari kuogelea, na aliwahi kuwa mmoja wa wachezaji wa timu ya wachezaji huko Hongkong. Wakati wanapokuwa na nafasi, baba yake hucheza mpira wa vinyoya na mama yake. Hivyo bibi Liu Zhangzhu na kaka yake mdogo wanaathiriwa sana na wazazi wao. Ingawa walijifunza kuogelea kutokana na matakwa ya baba yao, lakini bibi Liu Zhangzhu anapenda zaidi mpira wa kikapu, mpira wa vinyoya na mpira wa wavu, na kaka yake mdogo anapenda zaidi tenisi. Bibi Liu Zhangzhu alipozungumzia mchezo wa mafute, ambao unamsaidia apate mafanikio katika shughuli za michezo alisema, alianza kushughulikia mchezo huo baada ya kuhitimu kutoka chuo kikuu. Kwa kuwa anapenda sana shughuli za michezo, hivyo baada ya kustaafu bado anaendelea kushughulikia mambo hayo ya michezo. Bibi Liu Zhangzhu alisema,

    "Kama mimi na Bw. Guo Zhiliang, ingawa tunashughulikia kazi ya usimamizi ya michezo, lakini kusema kweli sisi ni watu wanaojitolea. Kama sisi hatukushughulikia mambo ya michezo wala hatupendi michezo, basi ni vigumu kwetu kushughulikia kazi hiyo kwa muda mrefu."

    Bibi Liu Zhangzhu alisema shirikisho kuu la michezo ni kama kampuni ndogo, hivyo watu wanaofanya kazi ya usimamizi wanapaswa kuzingatia mambo mbalimbali kwa upeo mpana zaidi, vilevile wanapaswa kushughulikia vizuri kazi mbalimbali ambazo ni pamoja na kuwasiliana na idara mbalimbali za serikali, kutafuta msaada kutoka wafanyabiashara na kushughulikia hisia za wachezaji.

    Bibi Liu Zhangzhu ni hodari kufanya kazi ya usimamizi, kwa mfano aliwaambia waandishi wa habari kwa mara nyingi kuwa una uwezekano mkubwa kwa wachezaji wa mashua zenye matanga, Wushu, mpira wa vinyoya, mpira wa meza, biliadi na mbio za baiskeli kupata medali, na mashindano ya mpira wa miguu na kuogelea ya kupokezana kwa wanawake wanne pia yana uwezekano wa kupata medali. Maneno hayo yaliwatilia moyo wachezaji. Katika siku ya kwanza ya mashindano ya Michezo ya Asia ya Guangzhou, mchezaji kutoka Hongkong bibi Li Huishi alivunja rekodi ya Asia kwenye mashindano ya mbio za baiskeli za mita 500 kwa wachezaji wanawake, na kupata medali ya dhahabu ya kwanza kwenye Michezo ya Asia ya Guangzhou.

    Licha ya kufanya kazi ya usimamizi kwa timu anayoongoza, bibi Liu Zhangzhu pia anafuatilia na kufanya juhudi kuhimiza maendeleo ya michezo ya Hongkong. Bibi Liu alisema,

    "Kwa kweli serikali ya Hongkong imeanza kutia maanani maendeleo ya michezo, na katika miaka ya hivi karibuni imetenga fedha nyingi zaidi katika mambo ya michezo, ili kuunga mkono maendeleo ya harakati za kuwaandaa wachezaji hodari na uenezi wa michezo. Serikali ya Hongkong inataka kuisaidia Hongkong kuendeleza harakati za kuwaandaa wachezaji hodari, na sisi sote tunaona kuwa michezo ni muhimu kwa ukuaji wa vijana."

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako