• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Mubarak aitisha mkutano kujadili hali ya uchumi

    (GMT+08:00) 2011-02-06 20:12:35

    Tarehe 5 Rais Hosni Mubarak wa Misri alifanya mkutano na waziri mkuu na baadhi ya mawaziri, ambapo wamejadili zaidi kuhusu athari mbaya ya maandamano kwa mambo ya uchumi, na namna ya kuhakikisha maisha ya kimsingi ya wananchi.

    Kwenye mkutano na waandishi wa habari, Waziri mkuu Ahmed Shafik amesema shughuli za uzalishaji kwenye jamii zimeanza kurudi katika hali ya kawaida, na Misri inapinga nchi yoyote kuingilia kati mambo yake ya ndani.

    Waziri wa fedha Bw. Ismail Radwan amesema, serikali itatoa kipaumbele katika kutatua tatizo la ukosefu wa ajira na kuongeza mapato ya watu, na makampuni ambayo miradi yao imecheleweshwa kutokana na maandamano hayatatozwa faini.

    Habari kutoka serikali ya Misri inasema rais Mubarak hajajiuzulu wadhifa wa mwenyekiti wa chama tawala cha National Democratic Party.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako