• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Barua 0315

    (GMT+08:00) 2011-03-15 16:27:20

    Msikilizaji wetu Mogire Machuki anuani ya baruapepe ni oscarmogire@yahoo.com anasema salamu za dhati kutoka kisii kenya. langu ni kuwasalimu kuwatakia kazi njema na pia kuitakia Jamhuri ya Watu wa China nyakati salama wanapojiandaa kuandaa mikutano miwili ya Bunge la umma na Baraza la mashauriano ya kisaisa hivi karibuni. Kila la kheri nawatakia wachina wawe na mkutano wa kupendeza na wenye manufaa duniani kote kama mwaka jana. kila lililo jema.

    Shukrani za dhati msikilizaji wetu Mogire Machuki kwa maoni yako, kwakweli mikutano hiyo unayosema ya bunge la umma la China na mkutano wa kamati ya mashauriano yote imefungwa na kwa ujumla yote imemalizika salama tena kwa mafanikio makubwa, ahsante sana.

    Msikilizaji wetu mwengine ni Mchana J. Mchana Salvatorian wa Morogoro Tanzania barua yake pepe ni mchanajo@yahoo.com naye anasema napenda kuungana na wananchi wa china wakiongozwa na watangazaji na viongozi wa radio China kimataifa kwa kuuaga mwaka wa chui na kuukaribisha mwaka mpya wa sungura kwanza nawapongeza wale wote walio uona mwaka mpya na pia nawaombea kwa mungu kwa wale waliojiandaa kuuona mwaka huu mpya, lakini mungu kawachukua dakika za mwisho. Pia napenda kuwajulisha wananchi wa china siku ya mkesha hamkukesha peke yenu bali na sisi marafiki zenu tulikuwa pamoja nanyi. Tarehe 2-2-2011 ni mkesha na tarehe 3-2-2011 ndio mwanzo wa mwaka kama nilivyo elewa. Ujumbe wangu uwe mwaka wa kujituma sio kusubiri kutumwa, maana yangu sio kusubiri hadi kiongozi wako akukumbushe la kufanya pia nisingependa kumsahau dada yetu mpendwa Pili Mwinyi kwa kumtakia safari njema kurudi nyumbani karibu sana utugawie mafanikio uliyo yapata huko China.

    Tunakushukuru sana Bwana Mchana J. Mchana kwa barua yako, mwaka wa chui milia ndio tumeshauaga na sasa tupo kwenye mwaka wa sungura, pia tumefurahi sana kusikia kuwa siku ya mkesha na nyiyi pia mlikesha pamoja nasi, hii inaonesha ushirikiano na mapenzi makubwa mliyonayo kwa wachina. Pia Pili naye anakushukuru sana kwa kumuombea safari yake iwe njema, kwani amekwenda na amerudi salama kabisa kama mnavyoweza kumsikia sauti yake leo hii kwenye kipindi hiki kipendwacho kabisa na wasikilizaji wote. Ahsante sana

    Sasa ni barua pepe ya msikilizaji wetu Franz Manko Ngogo

    rasmanko2003@yahoo.com anasema napenda niwape mkono wa heri kwa matangazo na heri njema mnaposherehekea mwaka mpya wa kichina. nimekuwa nyuma ya vipindi vyenu kwa kunufaika kwa vipindi vyenye maudhui na elimu nzuri kwa wasikilizaji wake. nasikitika kutosikia chochote kutoka kwa washindi wetu wa miaka 45 ya uhusiano wa kibalozi kati ya China na Tanzania. kitu gani walicho dharau na kukosa kuwavutia huko China na kubakia kimya? Stephen Magoye Kumalijah ni mmoja wa wale ambao wamekaa kimya. Mwezi Novemba nilienda Japan kwa ziara kama ilonileta China. hakika nimeamini kuwa China ni nchi inayoendelea na Tanzania bado haijaendelea! nnachosisitiza ni daraja kati ya CRI na wasikilizaji wake. tafadhali tembeleeni wasikilizaji. sisi kemogemba club, tuko tayari na twawakaribisha Tarime.

    Ahsante sana Bwana Franz Manko Ngogo kwa barua yako, mimi nafikiri baadhi ya washindi maalumu wa Chemsha bongo ya maadhimisho ya miaka 45 ya uhusiano wa kibalozi kati China na Tanzania hawajakaa kimya kwani toka warudi wanajitahidi kutuandikia, kwa mfano stepehen magoya amewahi kutuandikia si mara moja toka arudi sasa labda mawasiliano yenu binafsi, hilo hatutaweza kulijua. Hata hivyo tunafurahi sana kwani unaonesha jinsi gani unavyowajali wasikilizaji wenzako, ahsante sana.

    Na sasa ni zamu ya msikilizaji wetu Lenusi Kingalu wa Kihonda S.L.P 24 Morogoro Tanzania, naye ametuletea barua akisema leo nataka niipongeze serikali ya Italia kwa kugundua kinachoweza kusababisha laana katika taifa, kama kukosa mvua, magonjwa yasiyosikia dawa, kukosa mapato ya kukidhi mahitaji nk, ninazungumzia kitendo cha kupiga marufuku vimini na mavazi yote yasiyo na adabu kuonekana mahali popote nchini humo, na kama akipatikana mtu amevaa atatozwa faini au kwenda jela au kutumikia adhabu zote mbili hongera sana Italia naamini kwa hatua hiyo kama kweli mtaisimamia, mungu atawatendeeni maajabu makubwa.

    Pili nawapongeza madiwani na wabunge mliopata bahati ya kuingia katika nafasi hizo hapa nchini Tanzania, katika uchaguzi tulioumaliza hivi karibuni, na ninapenda niwape pole wale ambao hamjatimiza huduma kwa wananchi maana manung'uniko na maombi ya watanzania watakaokuwa hawapati huduma na kuonewa katika haki zao, yatamfikia muumba wetu nae atawatetea kwa kujilipiza kisasi. kuweni makini timizeni wajibu wenu kikamilifu. Hongera Tanzania, hongera viongozi wetu. Nawatakia sherehe njema za mwaka mpya wa jadi wa kichina ( mwaka wa sungura) zilizoanza hapo tarehe 2/2/2011-8/2/2011.

    Nilishtuka juzi niliposikia kipindi cha cheche zetu kinarushwa Jumatano, wakati kipindi hiki kinarushwa jumamosi. kumbe ni maalum kwaajili ya sherehe za mwaka mpya.

    Shukrani za dhati msikilizaji wetu Lenusi Kingalu kwa barua yako, sisi tunafikiri si Italia tu inayohitaji kufanya mageuzi hayo ya kudhibiti wale wote wanaopenda kwenda uchi, kwani siku hizi vijana wengi wanapenda sana kuvaa nusu uchi, hili ni jambo lisilopendeza, wasichana haohao ndio wanaolalamika kuhusu suala ubakaji, nafikiri wasichana wakianza kujihifadhi wenyewe basi hata wale wenye mtindo mchafu wa kuwakamata wasichana na kuwabaka basi watajisikia aibu, kwasababu wakati mwingine kile kitendo cha kwenda uchi ndicho kinachowatamanisha hao wabakaji. Wasichana tunakuombeni sana mjaribu kuvaa vazi la heshima ambalo litamtukuza mwanamke na sio kumdharaulisha. Ahsante sana.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako