Katika sehemu iliyopo umbali wa kilomita 10 kutoka Brega, waasi wamejenga ngome yao kwa kutumia mizinga na bunduki zinazobebwa kwenye magari. Mpiganaji mmoja alisema jumanne jeshi la Gaddafi liliwashambulia waasi walioko nje ya mji wa Brega kwa makombora na vifaru. Lakini NATO haijafanya mashambulizi kwa ndege kwa siku mbili, na waasi wamelazimika kurudi nyuma kutokana na kushambuliwa sana na jeshi la Gaddafi.
Ofisa mwandamizi wa NATO amesema, asilimia 30 ya jeshi la Gaddafi imeharibiwa katika mashambulizi yaliyoanza tarehe 19 Machi. Katibu mkuu wa NATO Bw. Anders Rasmussen jummane baada ya kukutana na Bw Jean Ping mwenyekiti wa kamati ya Umoja wa Afrika huko Brussels, alisema NATO na Umoja wa Afrika zimekubaliana kuwa Umoja wa Afrika unapaswa kufanya kazi muhimu katika utatuzi wa kisiasa wa mgogoro wa Libya.. Na baada ya hapo Bw. Jean Ping aliendelea na ziara yake nchini Italia, ambapo amekubaliana na waziri wa mambo ya nje wa Italia kuwa, ni lazima mapambano nchini Libya yamalizike na usimamishaji vita usimamiwe, raia wa kawaida walindwe, na kuandaa mazingira kwa ajili ya utatuzi wa kisiasa wa mgogoro huo.
© China Radio International.CRI. All Rights Reserved. 16A Shijingshan Road, Beijing, China. 100040 |