Marekani imetangaza kuuawa kwa mwanzilishi na kiongozi wa kundi la kigaidi la Al-Qaida Osama Bin Laden na kusema imeupata na inaushikilia mwili wake.
Osama anadaiwa kuuawa kwenye mashambulizi ya ardhini nje ya mji wa Islamabad kwenye nyumba yake. Katika hotuba yake, rais wa Marekani Barack Obama amesema kulitokea hali ya kufyatuliana risasi kati ya majeshi ya Marekani na wapiganaji.
Obama aliongeza kuwa Marekani imekuwa ikifuatilia habari kuhusu maficho ya Osama toka mwezi Agosti mwaka jana. Kwenye ripoti hizo ilibainika Osama alikuwa akijificha mjini Islamabad. Bin Laden alishutumiwa kwa kuhusika katika vitendo mbali mbali vya kigaidi duniani ikiwemo mashambulizi mjini New York na Washington Septemba 11 mwaka wa 2001.
© China Radio International.CRI. All Rights Reserved. 16A Shijingshan Road, Beijing, China. 100040 |