• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Barua za wasikilizaji

    (GMT+08:00) 2011-05-10 18:45:33

    Msikilizaji wetu Ras Franz Manko Ngogo wa Kemogemba Club, S.L.P 71, Tarime, Mara, Tanzania. Anasema ndugu wa Redio China Kimataifa, mimi binafsi kama msikilizaji ninayefuatilia matangazo yenu kwa karibu mno, nimekuwa nikikubali mfumo wenu tangu awali, kulingana na jinsi utamaduni na sera za taifa la China zinavyo waruhusu kufanya. Vipindi vyenye maudhui ya msimamo wa kadri na sera zenye mtizamo wa maendeleo kwa umma wa China na mataifa rafiki. Hayo yote yamenifanya niweze kuwa karibu na redio China kimataifa. Sasa mpango wa uboreshaji wa vipindi na matangazo kwa ujumla, hakika yameiweka CRI katika nafasi ya juu katika redio za kimataifa. Pengine CRI ikashika nafasi ya juu katika nyanja ya utangazaji kama inavyotia hofu katika nyanja ile ya uchumi na biashara duniani. Mimi mwenyewe sijaamini masikio yangu ninapokuwa naanza kusikiliza matangazo ya CRI kwa namna ambavyo hata taarifa ya habari inavyochanganywa na ripoti za matukio na waandishi wa CRI walioko maeneo mbalimbali ya ulimwengu. Nawatakia maendeleo murua ya uboreshaji wa vipindi, nami niko nyuma yenu.

    Barua nyingine inatoka kwa msikilizaji wetu Tabitha Khakali Akhusama wa S.L.P 2191 Kakamega Kenya, anasema mimi nikiwa kama shabiki wenu sugu na wa siku nyingi ningependa kutoa salamu zangu nyingi kwa watangazaji wote, wafanyakazi wote na wasikilizaji wote wa Redio China Kimataifa ulimwenguni. Napenda kutoa shukurani kwa redio yetu kwa kutuletea matangazo na vipindi kupitia KBC. Ningependa muongeze muda upande wa salamu, kutoka saa nne hadi saa tano, pia ningependa mnitumie kalenda ya mwaka 2011. Ahsanteni.

    Tunawashukuru sana wasikilizaji wetu Ras Franz Manko Ngogo na Tabitha Khakali Akhusama kwa barua, sisi tunawaahidi kuwa tutaendelea kuboresha matangazo yetu, na pia tunapenda kumjulisha Tabitha kuwa tutamtumia kalenda ya mwaka 2011. Ahsante sana.

    Na barua ya mwisho inatoka kwa msikilizaji wetu Mbarouk Msabah Mbarouk mwenye baruapepe mubarak_ghassani@hotmail.com naye ametuletea maoni kupitia kwenye tovuti yetu akisema ndugu watangazaji wapendwa, Katika kile ambacho wachunguzi mashuhuri wa maendeleo ya Sayansi na Teknologiya nchini Uingereza walivyotathmini hivi karibuni na kutoa taarifa yao juu ya uwezekano wa Jamhuri ya Watu wa China ikaweza kufika mbele zaidi katika kupiga hatua kubwa ya Maendeleo ya Sayansi na Teknolojiya na kuchukuwa nafasi ya mbele kabisa duniani nyuma ya Marekani katika kipindi cha muda wa miaka miwli tu ijayo , kwa kweli ni ushahidi wa kutosha ambao unadhihirishia Ulimwengu juu ya mafanikio makubwa yanayozidi kupatikana nchini China kwenye nyanja hiyo .

    Bila shaka yoyote kwa maoni yangu binafsi, athari kubwa za maendeleo hayo ya Kiuchumi kwenye nyanja ya Kisayansi na Kiteknolijiya ya China katika kila pembe ya dunia yetu ya leo, huenda ikawa ni sababu kuu ya kimsingi kwa Ulimwengu wa Magharibi kutanabahi kwamba nguvu na uwezo wa kusambaa kwa maendeleo hayo ni jambo lisiloweza kuepukika.

    Chini ya mazingira hayo Mataifa yanayoinukia hasa barani Afrika yana kila sababu ya kujikita katika ushirikiano wa karibu na Jamhuri ya Watu wa China kwa vile tumejaaliwa kuwa na maliasili nyingi ambazo tumeshindwa hadi leo kuzitumia vyema katika kukuza Uchumi na kujiletea maendeleo, ili kuweza kupiga hatua kama hiyo na kunufaika vyema na mbinu za kufaulu kujikwamuwa katika ukosefu wa maendeleo, ambazo China iliweza kuzitumia na hatimae kufikia malengo na hata kupindukia , basi hatuna budi kuwa na nia ya kweli ya kufanya hivyo kwani Wahenga walisema " penye nia pana njia ".

    Mwishoni ningezinasihi nchi zetu ya Kiafrika kuachana na dhana ya baadhi ya Mataifa Makubwa kwamba enzi hizi mpya za Ushirikiano wa Kimaendeleo kati ya China na Afrika umekuwa chini ya kivuli cha kutaka kupora raslimali zetu . Kwa kweli dhana hiyo isiyokuwa na msingi mimi naichukulia kama ni propoganda tu za kutaka kukwamisha Uhusiano huu mpya wa Kihistoria na cha msingi zaidi ni kwa Mataifa yetu ya Kiafrika kutumia vyema utajiri wa maliasili tulizonazo ili kujenga na kuboresha miundo mbinu itakayoweza kusaidia katika uzalishaji na hatimae na sisi tutaweza kupiga hatuwa kubwa ya Kimaendeleo kama wenzetu wa Jamhuri ya Watu wa China.

    Shukuran za dhati bwana Mbarouk Msabah Mbarouk kwa maoni yako, ni kweli China inajitahidi sana katika nyanja ya sayansi na teknolojia, na hii ndio sababu nchi za magharibi kuwa na wasiwasi mkubwa kwa hatua zinazopigwa na China, vilevile China haina malengo mabaya katika kuwekeza au kuzisaidia nchi za Afrika, kwani inatekeleza hatua zilizofikiwa kwenye baraza la ushirikiano kati ya China na Afrika, jambo muhimu ni kuzidisha mashirikiano. Ahsante sana.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako