Matangazo ya FM ya Radio China Kimataifa tarehe 20 yameanzishwa rasmi huko Bangui, mji mkuu wa Jamhuri ya Afrika ya Kati.
Kwenye sherehe ya uzinduzi wa matangazo hayo, waziri wa habari wa Jamhuri ya Afrika ya Kati Bw. Alfred Poloko amesema, uzinduzi wa matangazo hayo ya CRI ni muhimu sana kwa uhusiano kati ya Jamhuri ya Afrika ya Kati na China, serikali ya Jamhuri ya Afrika ya Kati na wananchi wake wanatarajia kujifunza uzoefu wa maendeleo ya uchumi wa China, na kutaka kuendeleza uhusiano wa kirafiki na China kwa kupitia matangazo ya CRI.
Matangazo hayo ya CRI yanatangazwa kwa lugha ya kifaransa kupitia wimbi la FM97.7.
© China Radio International.CRI. All Rights Reserved. 16A Shijingshan Road, Beijing, China. 100040 |