• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Lusaka-Zambia yafanya mazishi ya kitaifa ya aliyekuwa rais wa nchi hiyo Fredrick Chiluba

    (GMT+08:00) 2011-06-28 10:45:05
    Mazishi ya kitaifa ya aliyekuwa rais wa Zambia Fredrick Chiluba yamefanyika jana nchini humo.

    Ibada ya mazishi ilifanyika katika kanisa la Msalaba Mtakatifu mjini Lusaka na kuhudhuriwa na waombolezaji wengi wakiongozwa na viongozi wa serikali na mabalozi wa nchi mbalimbali.

    Miongoni mwa viongozi waliohudhuria mazishi hayo ni rais wan chi hiyo Rupiah Banda, rais Joseph Kabila wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo, rais wa zamani wa Tanzania Benjamin Mkapa na waziri mkuu wa Zimbabwe Morgan.

    Wakati huohuo, rais Jakaya Kikwete wa Tanzania ameungana na Wazambia katika kuomboleza kifo cha rais Chiluba. Amemwelezea Bw. Chiluba kuwa ni kiongozi atakaye thaminiwa daima barani Afrika, hususan katika jumuiya ya SADC.

    Ameihakikishia familia ya marehemu na Wazambia kwa ujumla kuwa Watanzania wako pamoja nao katika msiba huo. Rais Kikwete amesema hayo alipokuwa akisaini kitabu cha maombolezo katika ubalozi wa Zambia nchini Tanzania.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako