Hafla ya serikali ya China kukabidhi kituo cha vielelezo vya teknolojia za kilimo kwa serikali ya Msumbiji ilifanyika hiyo jana katika wilaya ya Boane mkoani Maputo, Msumbiji.
Waziri wa sayansi na teknolojia wa Msumbii Bw. Venancio Massingue alisema kuzinduliwa kwa kituo hicho ni uungaji mkono wenye nguvu kwa Msumbiji kutekeleza mpango wa kimkakati wa kuendeleza kilimo, na kituo hicho kitakuwa idara muhimu ya kufanya utafiti, kutoa mafunzo, kufanya uzalishaji na kutoa vielelezo vya teknolojia, na kitatoa mchango kwa ajili ya kuongeza uwezo wa uzalishaji wa kilimo nchini Msumbiji.
Balozi wa China nchini Msumbiji Bw. Huang Songpu alisema kituo hicho ni kimoja kati ya vituo 14 vya vielelezo vya teknolojia za kilimo vilivyojengwa kwa msaada wa China katika nchi za Afrika. Alisema kilimo ni sekta muhimu ya ushirikiano kati ya China na Msumbiji, na China inapenda kuisaidia Msumbiji kuongeza uzalishaji wa kilimo.
© China Radio International.CRI. All Rights Reserved. 16A Shijingshan Road, Beijing, China. 100040 |