• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Ubunifu ni njia moja ya kujieleza

    (GMT+08:00) 2011-07-11 20:15:44

    Akiwa amevaa miwani yenye fremu nyeusi, fulana nyeupe na raba, Bw Zhang haionekani kama yuko tofauti na wanamitindo wanaovaa nguo anazobuni. Imefika saa nane mchana, yeye na wanamitindo wake wanajiandaa kwa ajili ya maonyesho yake ya kwanza. .

    "kwanza ninatakiwa kukagua kama nguo hizo zinawafaa wanamitindo hawa. Nimewaambia waje kujaribu nguo walizochaguliwa, kama kuna matatizo yoyote, najaribu kufanya marekebisho."

    Maonyesho ya kwanza ya Zhang Da yalikuwa yatafanyika siku inayofuata, na aliichukulia siku hii kama ni giza kabla ya kupambazuka . Alitembea huku na kule na kuweka kumbukumbu za wanamitindo na nguo walizovaa. Baadhi ya wakati, alisita na kuwaangalia kwa karibu zaidi . Msaidizi wake alisema Bw Zhang alianza kufanya kazi saa tatu asubuhi, akiwasiliana na wanamitindo wote na washirika wake kuhusu onyesho la kesho. Alikunywa maji kidogo tu lakini hali chakula. Zhang Da anasema katika siku za kazi, kila siku anatumia saa 10 kwa wastani kufanya kazi ofisini mwake.

    "Nilifungua studio yangu miaka mitano iliyopita. Ingawa bado ni ndogo, lakini nafurahia jinsi mambo yanavyoenda. Nashughulikia ubunifu na wengine wananisaidia kuwasiliana na vyombo vya habari, kutafuta wawekezaji na kutengeneza nguo."

    Kampuni yake ina watu wasiozidi 20. Zhang Da anasema baadhi ya wakati, hana budi kushughulikia masuala madogo yeye mwenyewe, kama vile kulipa ankara ya umeme. Kuhusu vipi anapata msukumo wa ubunifu, Bw Zhang anasema si kama watu wengi wanavyofikiri kuwa hisia zinaibuka ghafla.

    "watu huwa wanaamini kuwa hisia ni kitu cha ajabu. Lakini ukweli ni kwamba hisia inatokana na mkusanyiko wa maarifa na ujuzi. Baadhi ya wakati, sina hisia hata kidogo, lakini wakati mwingine, mawazo mazuri sana yananijia akilini, hali hii ni ya kawaida kwa mbunifu. Sijatawaliwa sana na ubunifu . Nafurahia maisha yangu. Ubunifu ni kazi yangu tu."

    Bw Zhang Da anasema ingawa sasa ana chapa yake mwenyewe, lakini ametimiza asilimia 20 tu ya malengo aliyoyaweka. Akiwaangalia wanamitindo wake wakifanya majaribio ya kutembea kwenye jukwaa katika maonyesho yake, akisema anatarajia kuwa kampuni yake itakuwa kubwa na watu wengi watapenda nguo alizobuni.

    "kwa kweli, hili ni maonyesho yangu ya kwanza. Sikutarajia kufanya maonyesho ya mavazi nchini China ili kujitangaza. Niliwahi kubuni nguo zisizo za kawaida. Lakini nguo ninazoonyesha kwenye maonyesho hayo ni tofauti. Napenda kuzitumia kuonyesha suti za wafanyakazi wachina katika miaka ya 80. Na vilevile nataka kuchanganya sehemu za miji na vijiji nchini China."

    Sambamba na midundo yenye nguvu kusindikiza maonyesho hayo, wanamitindo wanatembea kwa madaha kwenye jukwaa na Zhang Da anawaangalia kwa makini, na anaweka mikono kifuani. Yeye ni mmoja wa wabunifu wa China, lakini ana ndoto zake. Tunaweza kuona matumaini, nia na malengo machoni mwake. Lakini bado hajapata mafaniko makubwa sana.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako