• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Mweledi wa Taichi-Liu Daiming

    (GMT+08:00) 2011-07-17 19:55:47

    Ni siku moja kwenye mwezi Agosti yenye ukungu na hewa ya unyevu. Mweledi wa Taichi, Liu Daiming mwenye umri wa miaka 38 anatoka mjini saa 3:30 asubuhi, akielekea kwenye uwanja uliojificha mbali na barabara. Leo atakuwa na darasa hapa.

    Siku hiyo mapema, anafanya mazoezi yake ya kila siku katika sehemu inayojulikana kama Temple of Heaven

    "naamka saa 12 asubuhi kila siku, mimi na marafiki zangu tunakwenda Temple of Heaven kufanya mazoezi ya Taichi. Hii inapendeza sana. Nakwenda pale kila siku."

    Mweledi huyo wa Taichi ana nadharia kuhusu kuamka mapema. Anaamini kuwa kwenye usanifu wa jadi wa kichina, Fengshui, unaohusiana na utamaduni wa Taichi, kuna elementi tano za kimsingi kwenye bahati ya watu na kwamba kuna njia fulani zinazoweza kuzisawazisha.

    "Nilizaliwa katika majira ya mpukutiko, ambapo watu waliozaliwa kwenye majira hayo huwa mwili wao una elementi ya dhahabu, na ni bora kufanya kazi wakati wa asubuhi. Kadri wanavyoamka mapema asubuhi, ndivyo wanavyokuwa na bahati katika siku hiyo"

    Haichukui muda mrefu kufika uwanjani hapo. Leo darasa hilo linafanyika juu ya jengo, eneo ambalo si mahali pa kawaida kufanya mazoezi ya Taichi. Eneo hilo linatumiwa sana kwani mnaweza kuona maeneo yenye njia nyembamba nyingi za jadi za kipekee za kichina, Hutong.

    Liu ana msingi imara kuhusu Taichi kwani alianza kujifunza Kung Fu alipokuwa na umri wa miaka 14. Aliwahi kushika nafasi ya kwanza kwenye mashindano ya kupiga ngumi ya Taichi Quan na kuchezea upanga wa Taichi jijini Beijing. Liu aliwahi kuacha kazi yake ya ukalimani, na kufundisha Taichi. Katika miaka ya hivi karibuni, ameendesha darasa moja la Taichi lilitwalo Zhang Sanfeng, ambaye anadhaniwa kuwa ni mwanzishi wa utamaduni wa Taichi.

    "Taichi imejulikana kwa watu wengi katika miaka ya karibuni. Na hata kuna filamu iliyoigizwa na Jet Li kuhusu mweledi huyo wa Taichi Zhang Sanfeng. Nawashauri wanafunzi wangu waingalie filamu hiyo wakiwa nyumbani, ili kupata picha kuhusu Taichi, hata hivyo kujiunga na madarasa kuhusu Taichi kutasaidia kuufahamu zaidi utamaduni wa kichina."

    Darasa la leo linahudhuriwa na wanafunzi saba kutoka Norway, ambao wako likizo na wanatembelea Beijing. Liu anasema faida kubwa kwa watu wanaojifunza Taichi ni kupumzika, kuwa na afya nzuri na kutulia kiakili. Kupata faida hizo kunatokana na mazoezi ya muda mrefu na yenye bidii. Kwa wanaojifunza Taichi kwa muda mfupi, Liu anatumia muda wa saa moja kujulisha utamaduni mpana. Hii si kazi rahisi, lakini ana njia yake yenyewe.

    "unatarajia kujifunza zaidi? Hebu tuangalie hatua tisa za Taichi. Weka miguu pamoja, viganja vitazame mbele na weak mikono juu"

    "nilibuni aina rahisi ya Taichi baada ya kuangalia hatua tisa. Wanafunzi wanaweza kujifunza zote kwa muda wa saa moja, na nitawajulisha kanuni za jumla za Taichi. Kawaida hatua ya kwanza nitatangulia kupiga Taichi kisha nitawaambia wanafunzazi hao waniige."

    "siku zote dumisha hali hiyo unapocheza Taichi. Nyosha mwili wako, ujisikie kama mwili wako unavutwa na mbingu na ardhi. Shusha mabega na vuta kifua. Usitanue kifua. Peleka mabega mbele kidogo."

    Liu Daiming anasema watu wengi wameanza kupenda utamaduni wa China, lakini wengi wa wageni hawafahamu Taichi kabla ya kuja China. Anatarajia kuwa kuhudhuria darasa lake kutaweza kuwapa wazo la jumla. Yeye ni hodari katika kufahamisha nadharia kuu za Taichi kwa njia rahisi, kwa ajili ya kulifanya kila darasa liwe na maana na lenye furaha.

    (sauti kwenye darasa)

    "-Hebu tusimame vizuri. Tunarudia mambo ambayo tumeshajifunza. Sasa nitawaacha mjaribu taratibu zote.

    - Lakini huenda hutafurahi.

    -Sawa. Nafanya mzaha tu. Usijali"

    Mwalimu na wanafunzi wote wanapenda sana darasa hillo bila ya kujali hewa ya unyevu. Mwishoni, Liu anafahamisha mambo yanayopaswa kuzingatiwa kwani wanafunzi wanapenda kufanya mazoezi zaidi ya Taichi baada ya kurudi nyumbani.

    "Kisha weka mguu wa kushoto nyuma kidogo. Huo ndio utaratibu wote. Bora mzijaribu bila kuongea hata neno moja au kusikiliza muziki. Kama ukiongea sana, utashindwa kujisikia upekee na utulivu. Taratibu hizo zinapaswa kufanywa katika mahali tulivu na hewa nzuri. Mahali penye watu wachache na miti mingi panafaa zaidi. Kuhusu kupumua, Taichi inazingatia pumzi ya asili. Unavuta na kutoa pumzi kwenye miondoko yako. Vuta pumzi ndefu na ya asili, ni hivyo tu. Natarajia nyinyi mnaweza kukumbuka leo. Mlikuwa China na kujifunza Taichi."

    Darasa hilo limemalizika. Liu Daiming anakula tambi ikiwa chakula cha mchana, halafu anakwenda kwenye njia yake tena. Hewa yenye unyevu inamfanya akaribie kushindwa kuvuta pumzi, lakini Liu anaendelea na shughuli zake. Anakwenda kukutana na mawakala wa usafiri, anatarajia kuongeza darasa la Taichi katika mpango wa safari.

    "sasa wanapanga njia za safari kwa mwaka kesho, hivyo siwezi kusubiri hadi mwezi ujao watakapomaliza mipango yao."

    Baadaye atakuwa na darasa jingine, na kutafuta wanafunzi wengine kutoka nchi mbalimbali duniani watakaopenda kujifunza Taichi. Anatarajia kuwa Taichi itakuwa mchezo wa kitaifa nchini China.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako