• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Siku ya kawaida ya mmiliki wa mgahawa

    (GMT+08:00) 2011-07-17 19:58:51

    Wang Jun mwenye umri wa miaka 32, anamiliki mgawaha mmoja uitwao Sky in Line uliopo Beijing, mji mkuu wa China. Ingawa ameishi Beijing kwa miaka mitano, lakini anajivunia sana kila wakati anapozungumzia maskani yake, mkoa wa Yunnan, kusini mwa China. Lakini maisha ya Wang Jun akiwa kazini kila siku yakoje? Tufuatane naye pamoja na mwandishi wetu wa habari kupata hisia ya siku nzima ya kazi za mmiliki wa mgahawa. .

    "mgahawa unafunguliwa saa tatu na nusu asubuhi, na wateja wanaweza kuagiza chakula baada ya saa nne aubuhi. Wafanyakazi wanakula chakula cha asubuhi kuanzia saa nne na nusu asubuhi, na chakula cha mchana kuanzia saa kumi na moja jioni. Hatuna wakati maalum kwa chakula cha jioni. Baadhi ya wakati, ni saa tatu usiku, wakati mwengine zaidi ya saa tatu."

    Huyo ni Wang Jun, mmiliki wa mgahawa mdogo wenye umaalumu wa Yunnan uitwao Sky in Line uliopo jijini Beijing. Kabla ya kuwa mmiliki wa mgahawa, alikuwa mfanyabiashara wa vyakula aliyeuza bidhaa kutoka Yunnan, mkoa ulio maskani yake. Lakini biashara haikuwa kubwa, hivyo Wang alianza kutafuta fursa nyingine.

    Katika muda wake wa ziada, Wang anapenda kuwapikia marafiki zake vyakula vya Yunnan. Marafiki hao walifurahia sana chakula hicho, hivyo alifikiria, kwa nini asifungue mgahawa wenye umaalumu wa Yunnan? Baada ya mwaka mmoja, alifungua mgahawa huo uitwao Sky in Line jijini Beijing.

    Anaanza kazi yake kila siku asubuhi kwa kwenda supamaketi kununua vyakula vibichi (fresh products) na viungo kwa ajili ya mgahawa wake.

    Leo saa nne asubuhi, Wang Jun anakwenda tena Supamaketi.

    "Nakuja hapa kila siku. Vitu vikuu kwa vyakula kama vile mboga vinasafirishwa hapa kutoka Yunnan. Lakini kwa samaki, ambaye anapaswa kuwa mbichi, nakwenda kununua supamaket kila siku. Kutokana na kuzingatia ubora wa ladha, nanunua samaki kati ya watatu na watano kwa siku, kwani nahitaji kuhakikisha kuwa samaki wote watauzwa."

    Ni saa tano asubuhi, baada ya kununua vitu, Wang anarudi kwenye mgahawa wake kusaidia kuandaa chakula cha mchana. Mgahawa huo ni mdogo, una mita za mraba 30 tu, wahudumu watatu na wapishi wawili. Mgahawa huo upo kwenye njia nyembamba huko Houhai, eneo ambalo linajulikana sana hapa Beijing kutokana na wingi wa bar na migahawa. Nyimbo za jadi ya Yunan, pambo nzuri na picha yenye mandhari ya Yunnan vinawafanya wateja wajisikie wako mkoani Yunnan. Bado ni mapema kwa chakula cha mchana, hivyo Wang anafanya ukaguzi kama kawaida, wakati akieleza ni kwa nini ameuita mgahawa huo "Sky in Line".

    "mmoja kati ya marafiki zangu alikuwa na ndoto kuhusu mgahawa wangu. Wakati ule, nilikuwa ninaandaa kufungua mgahawa, lakini sikuwa na uhakika niuite nini. Rafiki yangu aliniambia kuwa aliniona nikiwa na shughuli nyingi kwenye chumba kidogo, ambacho kinaonekana kama uzi. Vilevile unajua chakula maalumu mkoani Yunnan kinaitwa tambi inayotengenezwa kwa mpunga ambayo pia inaonekana kama uzi, hivyo niliamua ghafla jina la mgahawa uwe Sky in Line. Mapambo yote hapa yanatoka katika duka nililokuwa nalo awali, na pia wateja wanaweza kuyanunua kama wakiyapenda".

    Sasa ni saa tano na nusu adhuhuri, wateja wengi wanafika kwenye mgahawa huo kwa ajili ya kupata chakula kitamu. Wang sasa ana shughuli nyingi sana, anaenda na kurudi jiko na sehemu ya chakula akitoa huduma kwa wateja wake. Ingawa kiyoyozi kinafanya kazi, lakini jasho linaonekana usoni mwake.

    Wakati umeenda, na sasa ni saa nane mchana. Mgahawa unarudi kwenye hali ya kawaida. Wafanyakazi wanasafisha meza na Wang yuko kwenye kampyuta. Wang anasema kila mchana anatangaza mgahawa wake kwenye mtandao wa internet. Anatembelea www.dianping.com, tovuti inayohusu migawaha nchini China, ambapo watu wanaweza kueleza maoni yao kuhusu vyakula mbalimbali.

    "ningependa kujua kama kuna maoni kadhaa yanayotolewa na wateja wangu, na vilevile naongeza habari kadhaa. Sasa biashara inakuwa nzuri siku hadi siku, na nina mpango wa kuiongeza. Hivyo kama nitapata muda, nitakwenda kuangalia kama ninaweza kununua mapambo yanayowakilisha Yunan.

    Wang anasema ana marafiki wengi jijini Beijing, ambao wanatoka Yunnan. Wengi wao ni wafanyabiashara wanaouza bidhaa zenye umaalumu wa Yunnan. Wanakutana baadhi ya wakati na kuchukuliana kama wana familia.

    Mapenzi kwa mkoa wao ni topiki ya kudumu kwenye mazungumzo yao. Kama Wang, marafiki zake wanamiliki maduka au bar, lakini hawapati pesa nyingi. Hata hivyo, wanaona kuwa maisha yao yatakuwa mazuri kama wanaweza kuwapa wengine furaha.

    Usiku unakuja. Wang Jun anarudi kwenye mgahawa wake kuendelea na biashara.

    Sasa ni saa mbili usiku, Wang Jun bado anashughulikia wateja wake vizuri ili wanapoondoka katika mgahawa wake wawe wameshiba na wana furaha. Ingawa amechoka kidogo, lakini Wang anasema shughuli nyingi za siku zinamfurahisha.

    Sasa ni saa nne usiku, siku nyingine yenye shughuli nyingi inakaribia kumalizika. Wang anafunga mlango wa mgahawa wake na kurudi kwenye nyumba yake aliyopnga karibu na mgahawa wake.

    Wang anasema anafurahia maisha yake ya sasa. Jambo linalomfurahisha zaidi ni tabasabu usoni mwa wateja wake, ambao wanaona vyakula vyake ni vitamu.

    Kutokana na jina lake Sky in Line, Wang anatarajia kuwa anaweza kutangaza uzuri wa maskani yake kwa wateja wake.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako