• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Kama una baa iitwayo "If"

    (GMT+08:00) 2011-07-17 20:02:59

    Kama una pesa na wakati wa kutosha, ungefanya nini? Kama unapenda pombe, na una kipaji cha kutengeneza cocktails, ungefungua baa? Yang Jun ni mtu aliyeamua kufanya hivyo. Yeye ni mmiliki wa baa ndogo iliyopo kwenye mtaa mwembamba uitwao Beiluoguxiang jijini Beijing. Yang amekuwa mmiliki wa baa kwa miaka 10, ndoto yake kubwa ni kubuni vinywaji vyake mwenyewe vitakavyobakia kichwani kwa kila mteja. Sasa hebu tuambatane naye ili tuangalie siku moja kwenye maisha yake ikoje?

    Ukiingia kwenye baa yake, unaweza kuona maneno yanayong'aa kwenye ukuta yasemayo: "kama umeingia bila hadithi, utatunga hadithi moja kabla ya kuondoka.

    Baa hii iitwayo "Si. If" iko katikati ya mtaa wa Beiluoguxiang. Mmiliki wa baa hiyo ni mwanamume mwenye umri wa kati mwenye nguvu na ubunifu, na anapenda kuvaa mavazi ya kawaida. Watu huwa wanamwona akikaa mbele ya baa yake saa 7, ambako anaanza kazi za kila siku.

    "kwa jumla, hatuna kazi nyingi wakati tunapofungua baa hiyo saa 7 adhuhuri, hivyo wakati huo huwa namwomba Jack ambaye ni mkuu wa wafanyakazi anitengenezee kinywaji. Namwambia jinsi anakavyoweza kuongeza uwezo wake."

    Baa ya Yang ni ndogo, lakini imepambwa vizuri. Ina ghorofa mbili na sehemu ya chini. Kwa kuwa yeye anapenda sana muziki, sehemu ya chini huwa inatumika kwa ajili ya kuandaa sherehe, ambapo marafiki zake wanaburudika kwa muziki wa aina mbalimbali huku wakinywa vinywaji..

    "Kila mwezi, tunaandaa shughuli inayohusu jambo fulani, ambayo inategemea mambo maalumu yanayotokea mwezi huu. Kwa mfano, Siku ya Watoto Duniani itakuwa mwezi Juni, kwa hiyo tunaandaa shughuli iitwayo "kumbukumbu gani unayo ya utotoni mwako". Tuna tovuti yetu iitwayo catchsiif.blogbus.com, ambapo tunawaalika watu kutoa maoni yao. Mwishoni tutawaalika watu kumi walioshinda waje wakashiriki tafrija pamoja na vinywaji."

    Wakati Yang anazungumza, Jack amemaliza kuchanganya pombe. Anamwambia Yang aonje. Yang ana tabasamu kidogo na kusema kuwa Jack ni hodari katika kuwahudumia wateja, lakini anapaswa kujitahidi katika kutengeneza vinywaji. Anasema hawezi kuvumilia kama mtu atasema hajafurahishwa na vinywaji. Ikiwa ni moja ya kazi zake, anamfundisha Jack jinsi ya kutengeneza kahawa vizuri.

    "Unatakiwa kuangalia na kufuata hatua zote kwa makini. Sasa natengeneza kikombe cha kahawa aina ya mocha, kijiko kimoja na nusu cha mbegu za kahawa, usizidishe wala usipunguze. Halafu tunazisaga kabla ya kutumia mashine, unapaswa kurekebisha halijoto na kuhakikisha kuwa zimelowa kiasi cha kufaa kusagwa. Katika hali hii, mbegu zitakuwa na ladha nzuri. Kama hazijafikia kwenye hali inayotakiwa, kahawa haitakuwa nzuri. Ni vigumu kuwa mtengenezaji hodari wa kahawa. Baadhi ya wakati, hata mimi huwa nafanya makosa. Unapaswa kuichukulia mashinde ya kahawa kama familia yako, kuifahamu na kuipenda. Rafiki yangu mmoja ambaye ni hodari katika kuchanganya vinywaji vya kahawa aliniambia kuwa kila kinywaji cha kahawa ni sehemu ya sanaa"

    Labda Yang amezaliwa kuwa mhudumu wa baa. Kabla ya kumiliki baa yake mwenyewe, alifanya kazi ya ukarani katika meli. Kwa bahati, alikutana na mhudumu mmoja wa baa aliyekuwa na utaalam wa kipekee. Baada ya mwaka mmoja, aliacha kazi yake na kufungua baa yake ya kwanza jijini Beijing miaka kumi iliyopita. Anasema sababu yake ya kuwa mhudumu wa baa ni kuwa, anapochanganya vinywaji, anabuni kinywaji chochote anachotaka na kufurahia ladha yake.

    Baa yake iliyopo kwenye Beiluoguxiang ni baa yake ya pili jijini Beijing. Kila mmoja anavutiwa na mchanganyiko wa ajabu wa kahawa na maziwa. Kahawa aina ya mocha ina ladha nzuri, na kufunikwa na malai tamu, ni uchungu kidogo, lakini pia ina utamu.

    Kadiri muda unavyopita, ndivyo jua linawaka na mwanga wa jua unapita kwenye madirisha ya sebule. Ghorofa ya pili kwenye baa ya Yang, inaonekana kama ni duka la vitabu lenye roshani, ambapo watu wanaweza kuona mimea ya kijani. Yang anasema anapenda kufurahia pande zote za maisha, na mimea ni sehemu moja ya maisha yake.

    "napenda sana mimea hii. Katika muda wangu wa ziada, napendelea kwenda sokoni kuona kama kuna maua ninayoyapenda. Nimepanda zabibu kwenye paa la roshani. Natarajia kuwa nitapata mavuno Septemba."

    Yang anasema sababu iliyomfanya afungue baa kwenye mtaa wa Beiluoguxiang ni kwamba anapenda mazingira kwenye mtaa mdogo. Ingawa uko katikati ya Beijing, lakini umetulia, hali ambayo imewafanya watu wasahau mambo yanayowasumbua maishani. Anapenda sana kuwa huru na kuburudika, na wengi wa wateja wake wamevutiwa na mazingira ya baa yake. Yang anafurahi sana wateja na marafiki zake wanapokuja kwenye baa yake na kunywa vinywaji majira ya jioni.

    "ninapenda kutoa huduma nzuri kwa wateja wangu. Tumebuni pombe mbalimbali aina ya cocktails ya "If". Zinaitwa "If together" "If Love" "If Bye" na "If everything is just if". Kila mtu anazipenda. Kama unajaribu "If together", kitu kimoja utakachotambua ni harufu nzito-kama watu wawili wanakutana kwa mara ya kwanza, wanakuwa na hisia za kupendana. Halafu wanamaliza kunywa kinywaji, inaonekana kama ni maji tupu. Baada ya kuwa pamoja kwa miaka mingi, mapenzi yanapungua, lakini mapenzi bado yapo. Ni kama kunywa maji, hakuna mtu anayeweza kuishi bila maji."

    Siku moja imeisha. Yang anarudi nyumbani na kusubiri siku nyingine ianze.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako