• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Lagos-Dawa mpya ya kuzuia malaria yazinduliwa nchini Nigeria

    (GMT+08:00) 2011-08-05 09:52:40
    Dawa mpya ya kuzuia malaria Artequick ambayo ni kizazi cha nne cha muungano wa tiba aina ya Artemisinin inayotengenezwa nchini China imetambulishwa nchini Nigeria ili kudhibiti ongezeko la ugonjwa wa malaria nchini humo. Dawa hiyo iliyotengenezwa na Chuo Kikuu cha Guanzhou cha Madawa ya Kichina ni bora zaidi, kiasi kidogo cha sumu, na haina madhara makubwa kwa watumiaji kama zilivyo dawa nyingine za malaria. Inawaua zaidi ya asilimia 95 ya vijidudu  saa 24 baada ya kutumia Artequick. Shirika la Afya Duniani linaripoti kuwa malaria inasababisha vifo vya zaidi ya watu milioni moja duniani kila mwaka, wengi kati yao wakiwa watoto wenye umri wa chini ya miaka mitano kutoka barani Afrika.
    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako