• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Tripoli-Ban Ki-moon asisitiza kazi muhimu ya Umoja wa Mataifa nchini Libya baada ya vita

    (GMT+08:00) 2011-08-27 18:04:09

    Katibu mkuu wa Umoja wa Mataifa Bw. Ban Ki-moon amesema, umoja huo unapaswa kufanya kazi ya kuongoza shughuli za uratibu katika mchakato wa ukarabati wa Libya baada ya vita kumalizika.

    Bw. Ban Ki-Moon jana aliitisha mkutano kwa njia ya video kati ya wajumbe wa mashirika yanayohusika ya kikanda na kimataifa na kwa pamoja wamekubaliana kuwa kazi kubwa ambayo Umoja huo unapaswa kufanya ni kuwa na mpango thabiti na unaowezekana ili kuisaidia Libya baada ya vita. Wajumbe walioshiriki mkutano huo wanatoka katika mashirika na jumuiya mbalimbali zikiwemo Umoja wa Ulaya, Umoja wa Afrika, Umoja wa Nchi za Kiarabu na Shirika la Ushirikiano kati ya Nchi za Kiislamu.

    Baada ya mkutano huo, Bw. Ban Ki-moon alisema pande zote zimekubaliana kuwa Libya imeingia katika kipindi kipya na muhimu sana, na kusisitiza umuhimu wa utulivu wakati wa mpito nchini humo.

    Amesema Libya inakabiliwa na changamoto kubwa, na kwamba cha muhimu kwa sasa ni kumaliza mapambano na kurejesha utaratibu na utulivu wa jamii.

    Umoja wa Afrika umetoa taarifa ikielezea matumaini yake kuwa pande zinazohusika za Libya zitaanzisha serikali ya mpito inayoweza kuwakilisha maslahi ya pande zote mapema iwezekanavyo na kupata maafikiano ya kitaifa, na Umoja huo unapenda kuchangia mchakato wa kutimiza demokrasia na ukarabati nchini Libya.

    Mapambano kati ya jeshi la wapinzani la Baraza la Mpito la Libya na lile linalomtii Bw Muammar Gaddafi bado yanaendelea mjini Tripoli na katika sehemu nyingine nchini Libya. Wakati huo huo jeshi la Jumuiya ya NATO lilifanya mashambulizi ya anga dhidi ya jeshi la Gaddafi, na kuteketeza magari 29 ya kijeshi na kituo cha makamanda mjini Soult.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako