Katibu mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-moon, Jumatatu amepongeza uamuzi wa serikali ya Sudan wa kuwasamahe mashekhe watano, ambao walikuwa chini ya ulinzi wa jeshi la pamoja la Umoja wa Mataifa na Umoja wa Afrika UNAMID, tangu zizuke vurugu mwaka mmoja uliopita.
Mashekhe hao wamesamehewa Jumamosi na gavana wa jimbo la Darfur Kusini kabla ya sikukuu ya Iddi el Fitr wiki hii ili kusherehekea kumalizika kwa mwezi mtukufu wa ramadhani.
Awali mamlaka ya Darfur Kusini iliiomba UNAMID iwakabidhi mashekhe hao kwa mamlaka hiyo, lakini UNAMID haikufanya hivyo, ikisema jukumu lao ni kuhakikisha kuwa haki za mtu binafsi zinatimizwa wakati wote.
© China Radio International.CRI. All Rights Reserved. 16A Shijingshan Road, Beijing, China. 100040 |