• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Nairobi-Mshindi wa tuzo ya amani ya Nobel wa Kenya aaga dunia

    (GMT+08:00) 2011-09-26 20:16:15

    Mshindi wa tuzo ya Amani ya Nobel Prof Wangari Maathai ameaga dunia katika hospitali moja mjini Nairobi jana usiku alipokuwa akitibiwa ugonjwa wa saratani.

    Mwanaharakati huyo mashuhuri wa mazingira wa Kenya amefariki dunia akiwa na umri wa miaka 71 baada ya kugundulikuwa kuugua maradhi ya saratani Julai mwaka jana.

    Prof Maathai alipata tuzo ya amani ya Nobel mwaka wa 2004 kutokana na juhudi zake za kutetea mazingira. Marehemu ameacha watoto watatu, wawili wa kiume na mmoja wa kike.

    Mbali na kuwa Mwanaharakati wa Maswala ya Mazingira na haki za binadamu , Wangari Maathai pia alikuwa mwanasiasa shupavu. Amewahi kuhudumu kama Mbunge na Naibu waziri wa Mazingira nchini Kenya.

    Prof. Wangari Muta Maathai alianzisha vuguvugu la Green Belt mnamo mwaka 1977, ambapo alifanya kazi na wanawake kote nchini kuboresha maslahi yao na kuhifadhi mazingira.

    Alikuwa mtetezi mashuhuri wa matumizi bora ya maliasili . Shughuli zake pia zilitambuliwa mara kwa mara kote duniani.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako