• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Mazowe-Jiwe la msingi la ujenzi wa shule ya watoto yatima kwa msaada wa China nchini Zimbabwe lawekwa

    (GMT+08:00) 2011-11-04 18:14:23

    Ujenzi wa shule ya watoto yatima ya Iron Mask mjini Mazowe, Zimbabwe inayojengwa kwa msaada wa China jana asubuhi umezinduliwa, ambapo rais Robert Mugabe wa Zimbabwe na mkewe Bibi Grace Mugabe walihudhuria sherehe za kuweka jiwe la msingi.

    Kilele cha sherehe hizo kilifika baada ya rais Mugabe kusema kwa kichina "udumu milele urafiki kati ya China na Zimbabwe". Shule hiyo ya watoto yatima iko umbali wa kilomita 40 kaskazini mwa Harare, ambapo ujenzi wake utagharimu Yuan milioni 50, sawa na dola za Kimarekani milioni 7.7. Mradi huu ni moja ya miradi muhimu inayojengwa kwa msaada wa China, na unatarajiwa kukamilika ndani ya miezi 16. Shule hiyo itakayokuwa na uwezo wa kuchukua wanafunzi 900 itakuwa na vyumba 27 vya madarasa, maktaba, chumba cha usanii, chumba cha muziki, chumba cha kompyuta, pamoja na uwanja wa michezo. Itakuwa ni shule kubwa zaidi ya watoto yatima nchini Zimbabwe.

    Mke wa rais Bibi Grace Mugabe kwenye hotuba yake alisema idadi ya watu duniani imefikia bilioni 7, hivyo serikali za nchi mbalimbali zinapaswa kufikiri namna ya kukidhi mahitaji yao ya kila siku na kutoa mazingira ya maisha yaliyo ya haki. Shule hiyo si kama tu itabadilisha sura ya mji wa Mazowe, bali pia itabadilisha hatma ya maelfu ya watoto ili waweze kutimiza ndoto yao. Alisema, "sherehe hii kuweka jiwe la msingi inaashiria kuwa ujenzi wa shule umeanza, nafurahia kuwa uhusiano mzuri uliopo kati ya Zimbabwe na China unaweza kuwanufaisha watu wenye matatizo hasa watoto hao. Nataka kusema ufadhili unatokana na moyo wa dhati, si lazima kutoka kwa matajiri."

    Balozi wa China nchini Zimbabwe Bw. Xin Shunkang alisema Zimbabwe inazingatia sana elimu. China ikiwa rafiki wa dhati wa Zimbabwe itajitahidi kutoa msaada kwa Zimbabwe katika mambo ya elimu.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako