• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Barua 0906

    (GMT+08:00) 2011-11-11 16:18:18

    Wasikilizaji wapendwa tarehe 1 Septemba ilikuwa siku ya maadhimisho ya miaka 50 ya Idhaa ya Kiswahili ya CRI, ambapo shughuli za maadhimisho zilifanyika. Kwenye sherehe ya maadhimisho, mkurugenzi wa Idhaa ya Kiswahili Bibi Hanmen akiwa kwa niaba ya wafanyakazi wote wa Idhaa ya Kiswahili ya CRI ameahidi kuwa, idhaa hii itaendelea na juhudi za kuandaa vizuri vipindi vyetu ili kuwafurahisha wasikilizaji wetu.

    Na wasikilizaji wetu mbalimbali wametuletea barua kupongeza siku ya maadhimisho ya miaka 50 ya Idhaa ya Kiswahili ya CRI.

    Mathew Kiptoo, Kenya, anasema, Radio China Kimataifa imefanya maendeleo makubwa sana. Watu wanaoishi Kenya wanatumia Kiswahili kwa lugha ambayo wanaelewa sana. Kwa hivyo, matangazo yakitumiwa hapa China inapeperushwa hadi Kenya inakuwa rahisi sana kwao kuelewa kinachoendelea duniani, hasa China, ama nchi nyingine ziko karibu na China. Kwa sasa naona sana, nchi ya China na nchi kama vile Tanzania, Kenya na nchi nyingnine ambazo ziko Afrika, kuna urafiki na kuna ushirikiano fulani ambao unapanda kwa kazi. Haswa sasa hizi vile mnatangaza kwa Kiswahili, ama kwa lugha rahisi kwa watu wanaoishi huko kuelewa, kwa hivyo, ushirikiano utapanda juu, na mambo mengi yatatekelezwa sana kwa haraka. Sasa nataka kusema nataka kuishukuru Radio China Kimataifa, kwa sababu imepiga hatua kubwa.

    Bw. Mogire o machuki Kisii Kenya, E-mail

    Salamu za urafiki ziwafikie hapo beijing.

    Kutoka hapa kisii kenya nawatakia kila lililo jema mpotimiza miaka 50 ya mafanikio kwenye kuitangazia jamii ya kiswahili ulimwenguni kote .

    Kweli mda mrefu huu na mko na kila sababu ya kusherehekea kipindi hiki kwa namna moja au nyingine na pia kutushirikisha sisi wasikilizaji kwenye kipindi hiki

    Kwa miaka hamsini iliopita na kwa msikilizaji mwaminifu huenda tumeyafahamu mengi kuhusu taifa la china taifa ambalo liko na zaidi ya historia ya miaka elfu tano.

    Kweli twawapenda kwa moyo safi mlio nao na kwa kuwa karibu nasi kama wasikilizaji wenu wapendwa

    Aidha nawatakia mafanikio kenye shughuli zenu za kila siku na pia katika zile harakati ngumu za kuandaa vipindi.

    Asante

    Utunzi wa Mwanahabari aliye pia msanii na mshairi-Mombasa,Kenya Bw. Khamis Swaleh Darwesh : PONGEZI RADIO CHINA KIMATAIFA

    Nasimama mbele yenu,kwa furaha na bashasha,

    Nina machache mwenzenu,nataka yaporomosha,

    Nitaitumia mbinu,shairi kuwakilisha,

    Naipongeza Radio,ya China Kimataifa.

    Leo ni siku ya heri,katika haya maisha,

    Kituo kilicho shwari,kinachotuhabarisha,

    Ni kimetimu umri,hamsini kuadhimisha,

    Naipongeza Radio,ya China Kimataifa.

    Idhaa ya Kiswahili,ilianza peperusha,

    Matangazo aliali,tena yanonufaisha,

    Ikawa kwetu sahali,mengi ilitujulisha,

    Naipongeza Radio,ya China Kimataifa.

    Tarehe kama ya leo,matangazo ilirusha,

    Kwa lugha tuipendayo,inayotufaharisha,

    Tangu hapo hadi leo,hamsini mefikisha,

    Naipongeza Radio,ya China Kimataifa.

    Pongezi zangu hakika,nataka kuzifikisha,

    Wakurugenzi husika,makoja ninawavisha,

    Namba moja mumeshika,idhaa mwaiendesha,

    Naipongeza Radio,ya China Kimataifa.

    Munastahili taji,wahariri nawavisha,

    Pia watayarishaji,kila siku mwaboresha,

    Na nyie watangazaji,idhaa mwanawirisha,

    Naipongeza Radio,ya China Kimataifa.

    Mkono wa tahania,kwenu ninaunyoosha,

    Kongole nawapatia,CRI inatosha,

    Kofia nawavulia,gari vyema mwaendesha,

    Naipongeza Radio,ya China Kimataifa.

    Katu mbele sitasonga,kwa hapa nahitimisha,

    Siwezi yote kulonga,mengi nimeyabakisha,

    Saluti ninaipiga,na kichwa nainamisha,

    Naipongeza Radio,ya China Kimataifa.

    ADISON JN. GAMBA MOB Kenya

    1. Elfu moja na mia tisa, Na sabini na mbili nataja,

    Shuleni nilikuwa, La nne langu darasa,

    Nikaijua China, Barua nikaandika,

    Ni miaka makumi matano, Tangu club zianze.

    2. Ndani yake magazeti, kutoka China yakaja,

    Ujumbe yaliubeba, wa Gazeti la uarfiki,

    China na Tanzania, Ujamaa ukawa nguo,

    Ni miaka makumi matano, Tangu club zianze.

    3. Katu mi sikuchoka, Barua zangu kutuma,

    Chekundu kitabu kikaja, juu maandishi yanena,

    Zidumu fikra zake, M/kiti Mao Tse Tung,

    Ni miaka makumi matano, Tangu Club zianze.

    4. Nao Beji ikaja, Kutoka Peking China,

    Njano shaba rangi yake, Sonara wake makini,

    Picha ya kichwa chake, Mheshimiwa ndugu Mao,

    Ni miaka makumi matano, Tangu Club zianze.

    5. Barua zangu nikatuma, Na Urusi zikaenda,

    Nikapata magazeti, Ya Urusi leo nataja,

    Yote ya urafiki, Tanzania na Urusi,

    Ni miaka makumi matano, Tangu Club zianze.

    6. Wewe ninayekutaja, wakati huo uko wapi?,

    Jacob Magoa fundi Bengo, Pili Mwinyi na Mpunji,

    Karo na Sisiye Wasilwa, Johari naye Hamei,

    Ni miaka makumi matano, Tangu Club zianze.

    7. Na kama mlikuwepo, Wima hamkusimama,

    Te-Te-Te mlitembea, kuanguka matopeni,

    Vyakula mkalishwa, Kinda la ndege mfanowe,

    Ni miaka makumi matano, Tangu Club zianze.

    8. Nagano na Kemogemba, Nataja Gulam Karimu,

    Elfu moja na mia tisa, sitini na nne kataja,

    Yeye alianzia, Peking radio kataja,

    Dar ubalozini, Machache aliyasema,

    Ni miaka makukmi matano, Tangu cluba zianze.

    9. Tuli tumetulia, wakongwe wa Cri,

    Katu papara hatuna, Masikio Twayapunga,

    Ushindani usosifa, hatutaki hasilani,

    Ni miaka makumi matano, tangu club zianze.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako