• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Msichana wa kazi nchini China

    (GMT+08:00) 2012-02-08 20:16:42

    Katika siku za hivi karibuni, familia nyingi za mjini hapa China zinapenda kupata wafanyakazi wa nyumbani ili kusaidia shughuli zao nyumbani, lakini kuna malalamiko kuwa si rahisi kupata msichana mzuri wa kazi na gharama za kuwaajiri zinapanda. .

    Bibi Liao anayeishi jijini Beijing amepata msichana mpya wa kazi badala ya msichana aliyeondoka hivi karibuni. Katika miaka 10 iliyopita, Bibi Liao amekuwa anamwajiri msichana kumsaidia mume wake ambaye ni mgonjwa. Lakini anasema mshahara wa wasichana wa kazi unapanda taratibu katika miaka hii miwili.

    "Ukitafuta msichana wa kazi katika shirika moja utaambiwa kulipa kwa yuan 1,800 hadi 2,000 kwa mwezi, ama sivyo hawakubali. Tunajua si rahisi kwao kuondoka maskani yao na kufanya kazi mijini, hivyo tunajitahidi kuwaridhisha."

    Msichana aliyeondoka kwa Bibi Liao alikuwa analipwa yuan 1000 kila mwezi, hiyo ilikuwa ya mwaka jana, lakini kwa sasa, Bibi Liao anatakiwa kumlipa msichana mpya wa kazi mara mbili ya kiasi hicho.

    Mbali na kupanda kwa misharaha ya wasichana wa kazi, mshahara wa mtu anayefanya usafi wa nyumba, tena kwa saa, nao unapanda pia.

    Bibi Yang, mkazi mwingine wa Beijing, anasema huwa anaita mtu wa kusafisha nyumba mara mbili kwa wiki. "Awali nilimlipa Yuan 10 kwa saa, baadaye ilifikia yuan 12, kisha yuan 15, na sasa wanadai Yuan 20 kwa saa kusafisha nyumba."

    Kwa nini gharama za kumwajiri msichana wa kazi inapanda sana katika miaka ya hivi karibuni?

    Lin Fengqin ni meneja wa shirika moja linalotoa huduma ya kusafisha nyumba, na anasema sababu kuu ni kuwa, watu wachache kutoka sehemu za vijijini wana nia ya kufanya kazi hiyo mjini.

    "Kama wanaweza kupata yuan 1,000 au 2,000 katika maskani yao, nani anataka kuja Beijing kuwa msichana wa kazi nyumbani kwa watu wengine? Maisha ya vijijini yameboreka, na ni watu wachache tu wanaokuja mjini kutafuta kazi mijini. Ndiyo maana kuna mahitaji makubwa ya wasichana wa kazi, lakini hali halisi ni kwamba, gharama za kuwaajiri ni kubwa."

    Lin Fengqi anasema wasichana laki nne wa kazi wanahitajika kila mwaka jijini Beijing, lakini asilimia 20 hadi 30 ya mahitaji haya hayajatimizwa. Na kila ifikapo wakati wa sikukuu ya mwaka mpya wa jadi wa China, asilimia hii inaongezeka na kufikia 40, ambapo ni ngumu sana kupata wasichana wa kazi nyumbani, kwani wengi wameondoka mijini na kurudi maskani yao kukutana na jamaa zao kusherehekea sikukuu.

    Kuna sababu nyingine ya kupanda kwa gharama za kuajiri wasichana wa kazi wanaotoa huduma kwa kiwango cha juu. Naibu mkuu wa Shirikisho la Huduma ya Kazi za Nyumbani la Beijing Mu Lijie anafafanua,

    "Awali huduma waliyotoa wasichana wa kazi ilikuwa si kubwa. Kwa mfano, wakati wanapotunza mzee au mtoto mchanga, wanachohitaji kufanya ni kuhakikisha tu hawaumii na kuhakikisha wanakula. Lakini siku hizi mambo yamebadilika. Wasichana wa kazi wanatakiwa kujua namna ya kutumia vifaa vya umeme na kufahamu elimu ya awali ya watoto. Ndiyo maana mahitaji ya wasichana wa kazi wa kiwango cha juu yameongezeka."

    Mbali na mahitaji makubwa ya wasichana wa kazi, wasichana hao pia wamekuwa wakijitahidi kuwa na ujuzi zaidi na uwezo mkubwa kwa nia ya kupata kipato zaidi.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako