• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Watibet washerehekea mwaka mpya wa jadi

    (GMT+08:00) 2012-02-22 19:44:52

    Watibet milioni 5 wanaoishi katika sehemu mbalimbali nchini China wanasherehekea mwaka mpya wa jadi wa watibet. Uwanja uliopo mbele ya kasri la Polata umepambwa kwa maua mengi ya kupendeza, taa nyekundu na "chiema" kubwa, ambacho ni chakula cha jadi cha watibet. Shughuli za kidini pia zinafanyika ili kuomba baraka katika mwaka wa dragon wa maji kwa kalenda ya jadi ya watibet. Mjini Beijing mamia ya watu watibet na wasio watibet wameshiriki katika shughuli za kidini ya maadhimisho ya siku ya mwaka mpya wa kitibet katika hekalu la Yonghegong. Shughuli kama hizo pia zimeandaliwa na jumuiya za watu wa kabila la watibet wanaoishi mikoani Sichuan na Tibet. Sherehe za mwaka mpya kwa kalenda ya jadi ya kitibet zinaanza tarehe 29 ya mwezi wa mwisho na kuendelea kwa nusu mwezi.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako