• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • China yafikiria kuwa na sheria mpya ya uzalishaji usiochafua mazingira

    (GMT+08:00) 2012-02-27 18:53:55

    Halmashauri ya kudumu ya Bunge la Umma la China ambalo ni chombo cha utungaji sheria nchini China leo imeanza kujadili kwa mara ya pili muswada wa marekebisho ya sheria ya uzalishaji usio na uchafuzi wa mazingira.

    Katika kikao cha siku tatu cha halmashauri hiyo, wabunge wataangalia upya muswada huo uliofanyiwa mabadiliko muhimu machache kuendana na maoni mbalimbali yaliyokusanywa.

    Makamu mwenyekiti wa halmashauri hiyo Sun Anmin amesema muswada huo unaangalia maana halisi ya ufungaji wa bidhaa kupita kiasi, na maelekezo ya jinsi uzalishaji usiochafua mazingira utakavyofuatwa kwenye viwanda.

    Muswada huo pia unapendekeza mpangilio mpya wa uwajibikaji kati ya serikali kuu na serikali za mitaa, matumaini ya mafanikio ya mpango huo katika ngazi mbalimbali za utawala, na pia unaeleza bayana matumizi ya fedha kutoka serikali kuu.

    Mabadiliko mengine muhimu katika muswada huo ni kuongeza maneno mengine kama "uhifadhi wa rasilimali" na "ufanisi". Sheria inayotumika sasa inasisitiza zaidi kupunguza uchafuzi wa mazingira.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako