• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Maisha mapya kwa watu waliohamishwa kutoka makazi yao

    (GMT+08:00) 2012-02-29 16:22:37

    Mwaka 2001, China ilizindua mradi wa kuwahamisha watu walioishi kwenye mazingira ya asili ya hali mbaya katika mikoa ya Sichuan, Yunnan, na mikoa mingine iliyo magharibi mwa China, ambapo watu hao wamehamia sehemu ambazo huduma za usafiri, maji na umeme zinapatikana kirahisi, ili kuwawezesha kuondokana na umasikini mapema na kujiendeleza.

    Tian Lanzhu alikuwa mkazi wa tarafa ya Nuanshui, asubuhi na mapema alianza safari ya kupanda mlima, akapata shida kubwa kutokana na vijia vya mlimani vyenye unyevunyevu na utelezi na vinavyopinda, baada ya mwendo wa dakika 20, alikuta wakazi wengine wakiwa tayari wanaendelea na shughuli zao.

    Miamba ya mchanga aina ya feldspathic inaitwa kansa ya dunia, kwenye ardhi ya miamba hiyo, hakuna hata jani linaloweza kuota, vilevile linaweza kusababisha mmomonyoko wa ardhi baada ya upepo kuvuma na mvua kunyesha, na kusababisha udongo mchache ardhini unaotegemewa na viumbe mbalimbali. Aina hiyo ya ardhi ya miamba inaonekana zaidi katika tarafa ya Shuinuan, na ni vigumu kwa tarafa hiyo kuondokana na mazingira mabaya ya kimaumbile, hivyo shughuli za uzalishaji za wakulima zilikwama sana.

    Wu De, mkurugenzi wa idara ya uhifadhi wa maji mashambani ya wilaya ya Zhunge'er, mjini Erdos, kusini magharibi mwa China, anasema miamba ya aina ya feldspathic inachukua asilimia 50 ya ardhi ya tarafa ya Shuinuan, hali inayofanya mazingira ya kilimo na ufugaji wilayani humo kuwa mbaya, hivyo wastani wa kipato cha wakulima wa tarafa hiyo ni chini sana. Ndiyo maana mwaka 2009 serikali ya wilaya ya Zhunge'er iliwahamisha wakazi wote wa tarafa hiyo na kuwapeleka sehemu zenye mazingira bora zaidi.

    Tian Lanzhu anasema miaka mitatu iliyopita, walilazimika kuondoka kwenye makazi yao yaliyoko katika mazingira mabaya ya asili, lakini kamwe hawawezi kuacha kabisa maskani yao. Hivyo baada ya miaka mitatu walirudi na kuyashughulikia mazingira ya miamba ya aina ya feldspathic, na silaha yao ya siri ni kupanda miche ya hippophae rhamnoides.

    Mkazi mwingine wa tarafa ya Nuanshui Wang Haiqing anasema miche ya hippophae rhamnoides inaweza kuvumilia hali ya ukame, na inafaa kukua kwenye ardhi ya miamba ya aina ya feldspathic, na kupanda miche hiyo kunaweza kudhibiti mmomonyoko wa ardhi.

    Baada ya kupanda miche ya mti, Tian aliendelea kupanda mlima, miti ya feldspathic imesambaa mlimani na inatoa na matunda mekundu yanayotamanisha sana.

    Katika sehemu iliyo kilomita kadhaa kutoka hapa, wakulima wengine wanachuma matunda ya miti hiyo. Ma Fuxiao anasema, serikali ya tarafa hiyo ilinunua miche ya mti na kuwahamasisha wakulima waliotoka tarafa ya Nuanshui warudi maskani yao kupandikiza miche ili kubadilisha mazingira ya asili ya huko, na hivi sasa wanaweza kupata mara tatu ya kipato walichokuwa wanapata zamani kutokana na shughuli hiyo ya kupanda miti. Akisema:

    (sauti 4)

    "Hatupumziki mwaka mzima, awali watu wanne wa familia yetu, wastani wa kipato cha kila mtu haukuweza kufikia yuan elfu 6 au elfu 7 kila mwaka, lakini sasa kila mmoja wetu anaweza kupata yuan elfu 20 hata elfu 30."

    Kitu kinachowavutia zaidi ni kuwa, haki ya kutumia ardhi na misitu kwa mkataba haibadiliki, kila mtu anaweza kupata faida kutokana na miti iliyopandwa katika ardhi yake. Bw. Wu De anafafanua zaidi,

    (sauti 5)

    "Tunadumisha haki ya kutumia ardhi waliyonayo wakulima, baada ya kutekelezwa kwa mradi wa kuboresha mazingira ya asili, wakulima hao wanaweza kupata faida kutokana na shughuli zao za kupanda miti katika ardhi yao, huu ni msingi wa kuwaongezea mapato. Tunawahamasisha watu hao warudi maskani yao ya zamani, na kila mkulima anapanda miti katika ardhi yake."

    Tokea mwaka 2009 hadi 2011, watu wapatao zaidi ya elfu 13 wa tarafa ya Shuinuan walihama kutoka tarafa ya Nuanshui kwa sababu ya mazingira mabaya ya asili. Watu hao walihamishiwa katika sehemu ya makazi iliyojengwa kwa pamoja na serikali za wilaya za Nuanshui, Shagedu na Xuejiawan. Kila familia inaishi bure katika nyumba moja iliyojengwa na serikali. Mbali na kutoka vijijini hadi mijini, na kutoka nyumba isiyo ya ghorofa hadi nyumba ya ghorofa mbili, serikali iliwapa misaada halisi ya kila kitu, ili kuboresha maisha yao. Mkuu wa tarafa ya Nuanshui Yang Jiejun anasema,

    (sauti 7)

    "Tuliwapa nyumba, kazi, ruzuku pamoja na huduma ya jamii, na kuwaandalia mafunzo ya ajira, hali itakayowaongezea mapato ili waweze kuishi maisha mazuri na kujiendeleza. "

    Mradi huo wa kuwahamisha watu kutokana na mazingira ya hali mbaya ya asili uliwanufaisha sana wakulima na wafugaji walioishi katika sehemu zenye hali duni ya kiuchumi, huku watu hao pia wakiwa hawana budi kujitolea kwanza, lakini wanaamini kuwa baada ya kufanya juhudi za kupanda miti kwenye ardhi ya maskani yao ya zamani, mazingira ya makazi yao ya zamani yataboreka, na wanatamani kurudi maskani yao ya zamani kuishi kwa furaha kama mababu zao walivyoishi,katika miaka mingi iliyopita.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako