• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Wanahabari wa ndani na nchi za nje wafuatilia mikutano ya mwaka ya NPC na CPPCC

    (GMT+08:00) 2012-03-02 16:46:27

    Idadi ya waandishi wa habari waliojiandikisha kukusanya habari wakati wa mikutano ya mwaka 2012 ya Bunge la umma la China na Baraza la mashauriano ya kisiasa la China imezidi 3,000, kati yao takriban 900 wanatoka nchi za nje.

    Naibu mkurugenzi wa kituo cha habari cha mikutano hiyo Zhu Shouchen amesema, wengi wa waandishi hao wanatoka vyombo vya habari vya nchi za magharibi. Japan na Marekani kila moja imepeleka wanahabari zaidi ya 200, aidha kuna waandishi wengi wanatoka makundi ya kiuchumi yanayojitokeza ikiwemo Russia, India, Brazil na Afrika Kusini.

    Bw. Zhu pia amesema, kutokana na kuinuka kwa hadhi ya China duniani, jumuiya ya kimataifa na vyombo mbalimbali vya habari vinafuatilia zaidi China na mikutano hiyo miwili muhimu. Aidha, kufuatia ongezeko la idadi ya wachina wanaishi ng'ambo, vyombo vingi vya habari vya kichina vimeanzishwa katika nchi mbalimbali, na vinafuatilia sana mambo mbalimbali nchini China.

     

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako