• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Mkutano wa mwaka wa Baraza la mashauriano ya kisiasa la China wafunguliwa

    (GMT+08:00) 2012-03-03 15:53:35

    Mkutano wa mwaka wa Baraza la mashauriano ya kisiasa la umma la China umefunguliwa rasmi leo tarehe 3 hapa Beijing. Mkutano huo ni wa mwisho wa baraza hilo la awamu hii ya 11 ya muda wa miaka mitano.

    Viongozi wa chama na serikali wa China Hu Jintao, Wu Bangguo, Wen Jiabao, Jia Qinglin, Li Changchun, Xi Jinping, Li KeQiang, He Guoqiang na Zhou Yongkang wamehudhuria ufunguzi wa mkutano huo, ambapo wajumbe wa baraza hilo wapatao zaidi ya 2200 kutoka vyama na makundi mbalimbali, makabila na sekta mbalimbali wamehudhuria mkutano huo, na watasikiliza ripoti ya kazi ya Halamshauri ya kudumu ya baraza hilo atakayotoa spika wa baraza hilo Bw.Jia Qinglin.

    Katika siku 10 zijazo, wajumbe wa baraza hilo watafanya majadiliano na kutoa maoni na mapendekezo yao kuhusu sera muhimu zinazohusu sekta mbalimbali za siasa, uchumi na maisha ya jamii.

    Baraza la mashauriano ya kisiasa la umma la China ni chombo muhimu cha kufanya ushirikiano na mashauriano ya kisiasa kati ya vyama mbalimbali chini ya uongozi wa Chama cha Kikomunisti cha China, nalo ni njia moja muhimu ya kuenzi demokrasia ya ujamaa katika maisha ya siasa ya China. Baraza hilo liliundwa na wajumbe wa Chama cha Kikomunisti cha China, vyama vinane vya kidemokrasia, watu wasio na vyama, makundi ya kiraia, makabila madogomadogo, watu wa hali mbalimbali, ndugu wa Taiwan, Hongkong na Makau na wachina walioishi katika nchi za nje, pamoja na watu walioalikwa kwa mahsusi, hivyo baraza hilo lina msingi mkubwa wa uwakilishi kwenye jamii.

    Habari nyingine zinasema, mkutano na waandishi wa habari katika Mkutano wa 5 wa Bunge la 11 la umma la China utafanyika asubuhi ya tarehe 4 Machi, ambapo msemaji wa mkutano huo atafahamisha hali ya mkutano huo, na kujibu maswali ya waandishi wa habari. Radio China Kimataifa itatangaza moja kwa moja mkutano huo kwa lugha ya Kichina na Kiingereza, na matangazo hayo pia yatarushwa kwa kupitia tovuti za Kichina na Kiingereza kwenye mtandao wa internet.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako