• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Mkutano wa 5 wa Baraza la 11 la Bunge la umma la China utafunguliwa tarehe 5

    (GMT+08:00) 2012-03-04 18:59:01

    Msemaji wa Mkutano wa 5 wa Baraza la 11 la Bunge la umma la China Bw. Li Zhaoxing leo hapa Beijing amesema, mkutano huo wa mwaka utafunguliwa tarehe 5 na kufungwa tarehe 14, muda wake ni siku tisa na nusu, na mkutano huo una ajenda 10 zikiwemo ajenda za kusikiliza na kuthibitisha ripoti ya kazi ya serikali, kuthibitisha na kuidhinisha ripoti ya mpango na ripoti ya bajeti, kuthibisha mswada wa matekebisho ya sheria kuhusu uhalifu wa jinai, kusikiliza na kuthibitisha ripoti za kazi ya Halmashauri kuu ya Bunge la umma, ripoti ya kazi ya mahakama kuu ya umma na ripoti ya kazi ya Idara kuu ya uendeshaji wa mashitaka.

    Bw. Li Zhaoxing amesema, wakati wa mkutano huo wa bunge la umma, pia itaitishwa mikutano mbalimbali na waandishi wa habari, ambapo maofisa waandamizi wa idara husika za serikali ya China watajibu maswali ya waandishi wa habari kuhusu sera za kidiplomaia za China, uhusiano wa China na nchi za nje, maendeleo ya uchumi na jamii, sera za fedha, pamoja na kuhakikisha na kuboresha maisha ya wananchi.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako