• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Vyombo vya habari vya nje ya China vyafuatilia hotuba ya Jia Qinglin

    (GMT+08:00) 2012-03-04 19:28:53

    Mkutano wa mwaka wa baraza la mashauriano ya kisiasa la China ulifunguliwa jana hapa Beijing, huku vyombo vya habari nje ya China vikitoa ripoti mbalimbali kuhusu hotuba ya mwenyekiti wa baraza hilo Jia Qinglin,ambapo ripoti zao zinataja mara kwa mara uchumi na mageuzi ya China na maisha ya raia wa China, hali kadhalika kwa wataalamu na wasomi wa nchi mbalimbali .

    Shirika la Utangazaji la Uingereza BBC limemnukuu Bw. Jia Qinglin akisema, kuhimiza masikilizano na utulivu wa jamii ni jukumu kuu la baraza la mashauriano ya kisiasa la China.

    Shirika la habari la Japan Kyodo limesema Bw. Jia Qinglin amesisitiza kuwa baraza la mashauriano ya kisiasa la China linabeba jukumu kubwa katika kutekeleza mpango wa maendeleo wa miaka mitano (2011-2015).

    Nalo shirika la Habari la Ufaransa AFP limepongeza mchakato wa mageuzi ya mfumo wa matibabu nchini China na kusema China imepata maendeleo makubwa katika kuwawezesha watu wengi zaidi wapate huduma za matibabu na kuboresha hali ya bima ya matibabu.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako