Mwenyekiti wa Baraza la mpito la taifa linaloitawala Libya NTC Mustafa Abdul Jalil amelaani baadhi ya nchi za kiarabu kuunga mkono na kutuoa msaada wa fedha kwa waasi wa mashariki mwa Libya. Bw Jalilametoa kauli hiyo katika mkutano na waandishi wa habari uliofanyika jana mjini Tiripoli, baada ya viongozi wa kikabila na wanasiasa mashariki mwa nchi hiyo kutangaza Cyrenaica kuwa eneo linalojitawala.
Uamuzi huo wa eneo la Cyrenaica kuanza kujitawala ulitangazwa katika sherehe iliyofanyika mjini Benghazi na kuhudhuriwa na wajumbe 3,000, ambapo viongozi hao kutoka makabila na makundi ya kisiasa pia waliunda baraza la utawala wa eneo hilo chini ya uongozi wa Bw Ahmed Zubair al-Senussi. Bw. al-Senussi ameahidi kulinda haki ya eneo la Cyrenaica, lakini pia amekubali kuwa "baraza la mpito ya taifa la Libya" ni mwakilishi halali wa Libya kimataifa, Libya ni nchi moja na haitagawanyika.
Bw Jalil ameshutumu kuanzishwa kwa baraza hilo la kujitawala kama ni mwanzo wa njama dhidi ya Libya. Toka utawala wa Muammar Gaddafi upinduliwe, baadhi ya viongozi wa majimbo walikuwa wanatoa wito wa kurudishwa kwa mfumo wa shirikisho, uliofuatwa na Libya katikati ya karne iliyopita. Kutangaza kujitawala kwa Cyrenaica kunaweza kuathiri utawala baraza la mpito la taifa NTC katika sehemu ya mashariki ya nchi hiyo ambayo inajulikana kutokana na utajiri wa maliasili ya mafuta na kampuni kubwa zaidi ya mafuta ya petroli ya Libya ina makao makuu mjini Benghazi.
© China Radio International.CRI. All Rights Reserved. 16A Shijingshan Road, Beijing, China. 100040 |