• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Rais wa China asisitiza kuwepo kwa utulivu mkoani Tibet

    (GMT+08:00) 2012-03-09 19:38:01

    Rais Hu Jintao wa China amesisitiza kudumishwa kwa umoja wa kitaifa, mshikamano wa makabila na utulivu wa kijamii mkoani Tibet.

    Rais Hu amesema hayo alipokuwa akichangia mjadala wa wajumbe wa bunge la umma kutoka mkoa unaojiendesha wa Tibet katika kikao kinachoendelea cha Bunge la Umma la China. Amewataka watu waendelee kukusanya msingi thabiti kwa ajili ya kujenga Tibet mpya ya kijamaa.

    Rais Hu pia amesema kampeni ya muda mrefu ya elimu inatakiwa ihimizwe ili kuongeza mshikamano wa kikabila. Ametoa wito wa kuongeza juhudi za kuhakikisha maisha ya watu yanaboreka na kuinua huduma za jamii, ili makabila mbalimbali mkoani Tibet unufaike na matunda ya mageuzi na maendeleo.

    Aidha, rais Hu amesema mambo mengi yanatakiwa kufanyika ili kufanikisha maendeleo ya haraka katika sekta za kilimo, viwanda na huduma za biashara mkoani Tibet.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako