• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Napenda maskani yangu

    (GMT+08:00) 2012-03-12 09:02:18

    Bw. Zhu Xianmin ni mkurugenzi wa Shirikisho la Wapiga picha wa China. Lakini baada ya kufanya kazi ya kupiga picha kwa karibu nusu karne hapa China, Zhu anasema kamwe moyo wake haujawahi kwenda mbali na maskani yake. Anatumia upigaji picha kuonyesha mandhari ya kupendeza na watu wazuri wa maskani yake. Anatarajia kuwa watu wanaoangalia picha alizopiga wanaweza kupata kumbukumbu kuhusu hali halisi ya China na sura halisi ya Wachina. .

    Zhu Xianmin alizaliwa mkoani Henan kando ya Mto Manjano, katikati ya China. Anasema maskani yake ni sehemu yenye mandhari nzuri duniani na imempa kumbukumbu kubwa zisizosahaulika, hii ni sababu kuu inayomfanya Bw. Zhu apendelee kupiga picha watu na mandhari ya maskani yake.

    Zhu anasema alipokuwa kijana, yeye na wanakijiji wengine waliingiwa na hofu kila ifikapo majira ya joto.

    "Wakati ule, kila ifikapo miezi ya Agosti na Septemba, watu walioishi kando ya mto walikuwa na wasiwasi na mafuriko. Baadhi ya wakati, hata tuliogopa kusikiliza sauti ya mtiririko wa maji ya mto."

    Zhu anasema alipokuwa mdogo, watu wa maskani yake mara chache walijisikia wako salama. Wakati ule, hakukuwa na teknolojia ya kisasa ya kukinga mafuriko, hivyo ilikuwa ni rahisi kwa Zhu na wanakijiji wengine kuathiriwa na mafuriko. Kutokana na hatari inayojificha ya Mto Manjano, sehemu aliyokulia Zhu ilikuwa maskini sana na haikuendelea.

    "Nilipoondoka nyumbani kwa mara ya kwanza, sikujua taa ya umeme ni nini, na nilikula tufaha kwa mara ya kwanza nilipokuwa na umri wa miaka 20, na sikuamini kama kuna tunda zuri kama tufaha duniani."

    Alipotimiza miaka 17, kwa mara ya kwanza Zhu aliondoka nyumbani kwake na kujitahidi kutimiza ndoto yake ya kuwa mpiga picha hodari. Anasema kamwe hatasahau maneno aliyoambiwa na mama yake "kamwe usifanya mambo mabaya; na wala kuwadhuru wengine."

    Kwa Bw. Zhu bila kujali alifikia umri gani au kusafiri mahali gani, moyo wake siku zote ulikuwa kwenye maskani yake. Alipoanza kufanya kazi ya kupiga picha, alimpiga picha mkazi mmoja aliyeishi kando ya Mto Manjano akivaa skafu kichwani na fulana nyeupe na kuangalia mto huo. Ni wakati huo ambapo Zhu aligundua kuwa, kupiga picha za watu na sehemu anazofahamu zaidi itakuwa ni jukumu lake katika maisha yake yote.

    "napenda sana maskani yangu, kila ninapopiga picha najiuliza jinsi ninavyoweza kuonyesha vizuri maskani yangu ili watu wengine waone uzuri wake."

    Zhu anasema watu wa kwao ni wazuri, wenye hali ya kawaida na waaminifu, na wengi wao hawajawahi kupigwa picha. Zhu anataka kutumia kamera yake kukumbuka muda muhimu na hisia zisizosahaulika kwenye nyuso za watu ambazo zinaonesha mabadiliko na maendeleo yaliyopatikana katika maskani yake.

    Zhu anasema zamani, wakulima walioishi kando ya Mto Manjano walikuwa na wasiwasi na hali mbaya ya hewa, na ilikuwa ni vigumu kuona mashamba ya kijani, badala yake ni ukingo ulikuwa mkame.

    Lakini sasa hali imebadilika, kamwe hawaoni wasiwasi kwani wanatumia teknolojia kuwasaidia kurutubisha mashamba yao.

    "Kitu kimebadilika sana, awali watu walipanda baiskeli, lakini sasa watu wengi wamenunua magari. Miaka kumi iliyopita, hakuna mtu aliyeweza kujua kama daraja lingeweza kujengwa juu ya Mto Manjano. Nafurahia mabadiliko haya, na ningependa kuwa mtu anayeyakumbuka."

    Zhu Xianmin anasisimka sana anapozungumzia mabadiliko hayo makubwa yaliyopatikana katika sehemu ya kwao miaka 30 iliyopita. Machoni mwa watu wengi, Bw. Zhu sio tu ni mpiga picha hodari, bali pia ni mwangalizi wa jamii hiyo. Ana kumbukumbu ya miaka iliyopita na ataendelea kutumia kamera yake kukumbuka miaka ijayo na kuonesha uzuri wa sehemu na watu anaopenda zaidi.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako