• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Ren Qiang na gita yake

    (GMT+08:00) 2012-03-20 18:48:46

    Hiki ni kibwagizo cha gita cha sehemu ya mwanzo ya wimbo maarufu uitwao"California Hotel". Kwa vijana wengi, gita ni ala ya muziki ambayo ni rahisi kuiona na kuipata. Katika majira ya mchipuko, huwa tunawaona vijana wamekaa chini ya miti wakipiga gita huku wakiimba nyimbo mbalimbali.

    Ren Qiang anaishi katika chumba kimoja chenye mita sita za mraba katika nyumba iliyojengwa zamani kaskazini mwa Beijing. Yeye ana magitaa manane, na anasema anayatunza sana kwani kila gita linasimulia hadithi yake. Anasema, "Gita ni kitu chenye thamani kwa wale wanaoifahamu, lakini kwa watu wasioifahamu, gita ni mbao tu."

    Ren Qiang anafahamu sana gita. Ameishi hapa Beijing kwa miaka mitano tangu aondoke maskani yake mkoani Shanxi, kaskazini magharibi mwa China. Si jambo rahisi kwa Ren kununua gita hizo kutokana na kipato chake cha yuan elfu 3 kwa mwezi.

    Ren Qiang alianza kupenda gita alipokuwa mwanafunzi katika shule ya sekondari, jamaa zake wote walimpinga isipokuwa baba yake. Babu yake alisema hakuna mwanafamilia yeyote anayehusika na muziki, na mpaka sasa mama yake bado anaendelea kumshawishi arudi nyumbani, kwani akiishi nyumbani kwake, hatakuwa na haja ya kutafuta maisha .

    Mwaka 2005 Ren Qiang alihitimu kozi ya microelectronics na kupata kazi yenye mshahara wa yuan elfu 5 kwa mwezi, lakini rafiki wa rafiki yake alimtambulishia Ren kwa mpiga gita hodari nchini China Gao Jun, bila kujali pingamizi ya jamaa na marafiki zake, Ren Qiang aliacha vitu vyote nyumbani na kuja Beijing kujifunza kutoka kwa mwalimu huyo wa gita."Mwanzoni nilipokuja Beijing nilipanga nyumba kwenye ghorofa ya chini ya ardhi karibu na nyumba ya mwalimu wangu, baadaye nilimfuata rafiki yangu na tulipanga nyumba kwa pamoja. Sijawahi kujutia uamuzi huo ila tu nafanya bidii kufanya mazoezi ya kupiga gita."

    Ren anasema anapopiga muziki kwa gita mara kwa mara anaweza kukumbuka wazazi wa nyumbani, kuwazawaza udongo mnene kwenye uwanda wa juu wa maskani yake, ambpo kuna anga ya bluu na vijia vinavyoelekea mbali. "Nakumbuka wakati ule niliwahi kufanya mazoezi ya kupiga muziki kwa gitaa, nilipiga kwa zaidi ya mara mia kadhaa, lakini sikuchoka kabisa, na kila nilipopiga nilikumbuka sana maskani yangu. Kwani muziki huu uliweza kugusa sana hisia zangu juu ya maskani yangu, ambapo naweza kukumbuka mara kwa mara kuhusu bundi na kunguru walivyorukaruka kwenye milima katika maskani yangu Shanbei."

    Hata hivyo Ren Qiang hataki kurudi nyumbani, kwani anaona Beijing ni mahali anapoweza kutimiza ndoto yake, ambapo njia ya kuelekea kwenye mafanikio si ngumu sana. Ingawa katika miaka mitatu ya mwanzo Ren Qiang aliishi maisha magumu, lakini kwa bahati mwishoni mwa mwaka 2007 alipata fursa ya kujitokeza, ambapo kwa mara ya kwanza alishiriki katika shindano la kitaifa la upigaji gitaa na kuchukua nafasi ya kwanza, hii ilimfanya ajulikane miongoni mwa wapiga gitaa hapa China. Lakini ni yeye na wazazi wake tu wanaojua wanafanya juhudi namna gani katika kununua gitaa. Kabla ya shindano hili, wazazi wake walimnunulia gita moja ambayo bei yake ni yuan laki moja. Hii ni gita iliyotengenezwa kwa mikono nchini Marekani, je, kwa nini Ren Qiang aliinunua? Sababu yake ni rahisi sana. "Wakati ule, niliona ni gita hii tu inayoweza kueleza vizuri muziki fulani, naipenda sana. Gita hiyo ilitengenezwa kwa mikono, hivyo inauzwa kwa bei ghali sana."

    Baada ya kushinda kwenye shindano hilo, Ren Qiang alianza kupata fursa za kufanya maonesho katika klabu na miji mbalimbali ya China, pamoja na kipato anachopata kutokana na kufundisha upigaji gitaa, pia anaweza kujikimu kimaisha. Ren Qiang havuti sigara, hanywi pombe, havai nguo za kifahari, bali anaweka akiba ili anunue gitaa.

    Siku zote Ren Qiang anajitahidi kutimiza ndoto yake, ambapo amepata mafanikio, marafiki na mchumba wake. Hivi sasa, watu wanaokuja jijini Beijing ili kutimiza ndoto zao wanaongezeka, na wanatarajia kupata mafanikio kwa jasho lao. Inaaminika kuwa, katika karne hiyo kuna fursa nyingi zinawasubiri vijana hao.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako