• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Rais Wade wa Senegal akubali kushindwa

    (GMT+08:00) 2012-03-26 17:02:48

    Rais Abdoulaye Wade wa Senegal amekubali kushindwa kwenye duru ya pili ya uchaguzi wa rais wa Senegal iliyofanyika jana, na kumpongeza mpinzani wake ambaye ni waziri Mkuu wa zamani wa nchi hiyo Bw Macky Sall kwa kuwa mshindi. Matokeo ya Awali yanaonesha kuwa Bw Sall alikuwa anaongoza kwa kupata asilimia 69 ya kura huku Rais Wade akiwa na asilimia 30.84, watu zaidi ya milioni 8 walijiandikisha kupiga kura.

    Wakati wa kampeni Bw Wade aliahidi kuwa kama atachaguliwa kuwa rais ataanzisha utaratibu wa huduma za jamii kwa watu wote, utaratibu wa kutoa mikopo, huduma za matibabu na kuboresha mafao ya wastaafu. Pia alisema ataongeza nafakasi za ajira kwa vijana na kuwekeza zaidi ya dola za kimarekani bilioni 4 kwa ajili ya maendeleo vijijini, na pia kupunguza bei za bidhaa na vyakula vya msingi.

    Bw Wade aliingia madarakani mwaka 2000, na kuchaguliwa tena mwaka 2007. Uamuzi wake wa kugombea urais kwa kipindi cha tatu uliwafanya wapinzani kumshutumu kwa kukiuka katiba inayomtaka Rais awe madarakani kwa vipindi viwili.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako