• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Maua yanachanua katika uwanda wa juu wa Qinghai-Tibet

    (GMT+08:00) 2012-04-02 16:44:21

    Uwanda wa juu wa Qinghai-Tibet una mwinuko mkubwa kutoka usawa wa bahari, ambapo nyuzi joto ziko tofauti sana kati ya usiku na mchana, nuru ya miali isiyoonekana Ultraviolet ni mikali, ambapo hali ya huko ni ya ukame na yenye uhaba wa mvua, hali hii ambayo haifai kwa kazi ya kilimo. Watu wanasema, watu wanaoishi kwenye uwanda wa juu wanapenda sana maua kutokana na uchache wake katika uwanda huo, hivyo unapotembea mitaani mbalimbali katika uwanda huo, utaona maua ya aina mbalimbali kwenye vyungu yakichanua vizuri katika roshani ya nyumba za wakazi wa huko. .

    Sang Zhen ni mkazi wa eneo la Chengguan, mjini Lhasa, mkoani Tibet, katika ua wa nyumbani kwake, yeye na mume wake wamepanda maua ya waridi za kitibet, alizeti na zabibu na maua mengine, ua wake kama ni bustani moja ndogo. Anasema baada ya kustaafu, bustani hiyo imekuwa inawapa furaha tele yeye na mume wake. Akisema,

    "Tunafurahi sana. Katika ua wetu, tunaweza kupumzika, tunashughulikia maua hayo, tunasoma magazeti na kunywa chai. Butani yangu ina komamanga, zabibu na waridi. Waridi ya aina hii ni rahisi kupanda. Sasa maendeleo ya kiteknolojia yamepatikana, tunaweza kupata mbolea wa kufaa, na ardhi kwenye uwanda wa juu pia zimerutubishwa."

    Katika miaka ya 80 ya karne iliyopita, ilikuwa ni vigumu hata kupanda mboga mkoani Tibet, na maua yaliyopandwa yalikuwa ni ya kawaida tu, maua ya kifahari kama vile mawaridi hayakuweza kustawi, na maduka ya kuuza maua yalikuwa machache sana. Katika miaka ya hivi karibuni, kutokana na maendeleo yaliyopatikana katika uchumi na jamii mkoani Tibet, maduka ya kuuza maua yanaongezeka, na maua ya waridi pia yamekuwa vitu visivyokosekana katika maisha ya wakazi wa huko.

    Bi. Wang ni mmiliki wa duka moja la kuuza maua mjini Lhasa. Anasema duka lake linauza kwa wingi maua ya kifahari, na biashara yake ni nzuri, maua ya Waridi anayouza yanatoka mkoani Tibet, hivyo gharama ya uchukuzi wa maua imepungua. Awali waridi moja liliuzwa kwa yuan 80 lakini sasa ni yuan 10 tu, hii ni sababu inayoyafanya maua ya kifahari yanunuliwe sana na wakazi wa kawaida wa huko. Bi. Wang anashangaa sana kama maua hayo yanaweza kupandwa mkoani Tibet. Akisema,

    "Kabla ya kuja hapa, nilijua kuwa hakuna mimea inayoweza kukua kwenye ardhi ya Tibet, hali kadhalika kwa miti na maua milimani, sembuse mboga na maua mengi tunayoyaona siku hizi. Sikudhani kuwa mawaridi yanaweza kukua hapa."

    Asilimia 80 ya mawaridi katika soko la Lhasa yanatoka katika wilaya ya Duilongdeqing ya kitongoji cha Lhasa,. Wilaya hiyo ilijulikana kwa kilimo cha mboga. Kutokana na mahitaji makubwa ya soko, tangu mwaka 2007, kwa msaada wa serikali, wataalamu wa maua walienda wilayani hapo na kujaribu kupanda mawaridi kwa kutumia teknolojia, na hatimaye walipata mafanikio, hii si kama tu ilifungua mlango wa soko la mboga wa wilaya hiyo, bali pia imefungua soko la maua mjini Lhasa, na kufanya watu wengi zaidi kuwekeza katika kilimo cha maua.

    Lai Bingxu ni mtaalamu wa maua aliyekwenda Lhasa kutokana na mradi wa kuvutia mitaji na wawekezaji. Mtu wa kawaida anaweza kudhani kuwa hali ya hewa mkoani Tibet haifai kwa kilimo cha maua, lakini Bw. Lai anasifu hali ya hewa ya Tibet. Akisema,

    "Mwanga wa jua mkoani Tibet ni mzuri zaidi duniani, unajua mwanga wa jua ni muhimu kwa mimea kukua, hivyo maua yanayopandwa mkoani Tibet yanapendeza zaidi kuliko maua ya sehemu nyingine, rangi yake inadumu kwa muda mrefu, na vilevile ubichi wa maua hayo unaweza kudumu."

    Mkurugenzi wa ushirika wa wakulima wa mboga wa Gangdelin, wilayani Duilongdeqing Bw. Awangciren anasema,

    "Mtu mmoja anaweza kupata yuan elfu 12,000 kwa kupanda nafaka kwenye shamba la hekta moja, lakini akipanda mboga anapata laki moja na elfu 87.5, lakini mapato yanayotokana na maua ni mara mbili kuliko ya mboga. Ufanisi wa kupanda maua ni mkubwa sana, siku hizi upandaji wa maua unaweza kuwapa watu wa kawaida mapato ya yuan elfu 18 kwa mwaka."

    Tibet iko kwenye uwanda wa juu ambapo ni sehemu yenye baridi kali, na kuna mimea michache, lakini kutokana na juhudi zilizofanywa na watu wa kizazi baada ya kizazi katika kilimo cha mboga na maua, watibet wameweza kukidhi mahitaji yao ya kimaisha, vilevile maisha yao yanaboreka siku hadi siku. Mawaridi yaliyoingia katika soko la watibet taratibu, si kama tu yameboresha maisha ya watu, bali pia yameonesha mchakato wa maendeleo mkoani Tibet.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako