• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Shule ya msingi ya bweni mlimani

    (GMT+08:00) 2012-04-09 14:00:21

    Tarafa ya Maryang iko kusini mashariki mwa wilaya ya Tashkurgan Tajik, mkoani Xinjiang, China, ambapo ni sehemu yenye mwinuko wa mita elfu 3.1 kutoka usawa wa bahari, na. Tarafa ya Maryang imezungukwa na milima, na mto Yarkant na tawi lake Maryang unapita ndani yake. ..

    Katika tarafa ya Maryang, kuna familia 292 tu ambazo watu wengi familia hizo ni wa kabila la Watajik. Ili kuwawezesha watoto wote wenye umri wa kwenda shule wapate elimu, tarafa hiyo ilijenga shule moja ya bweni, lakini watoto wa vijiji vinne vya tarafa hiyo wanapata taabu sana kwenda shule. Kila muhula mpya wa masomo unapoanza, ndipo inapombidi Guo Yukun, katibu wa kamati ya chama ya tarafa ya Maryang aende katika vijiji mbalimbali kuwachukua watoto ili kuwapeleka shule. Anasema,

    "Kijiji cha Pili kiko kilomita 80 kutoka tarafani, na ni kijiji kilichopo mbali zaidi kati ya vijiji vinne vya tarafa hii. Tunakwenda kuwachukua watoto ili kuhakikisha wote wanaenda shule, kwani wazazi wengi hawataki watoto wao wasome, hivyo tunatakiwa kuwashawishi wazazi hao."

    Hakuna barabara inayounganisha tarafa ya Maryang na vijiji mbalimbali, hivyo ni taabu kuwapeleka watoto shule, kwani inawabidi wapande milima na kuvuka mito yenye maji baridi. Baadhi ya watoto wenye umri mdogo wanapopanda ngamia wanalia kwa hofu ya kuanguka kwenye mto. Bw. Guo Yukun anasema,

    "Kuna sehemu inayoitwa Miskong katika kijiji cha Pili, kutokana na maji mengi katika mto, ni mwezi wa pili na wa tatu tu ndipo watu wanapoweza kuingia na kutoka katika sehemu hiyo, nakumbuka hadi kufikia mwezi Aprili mwaka 2009, watoto 18 wa sehemu hiyo walikuwa hawajaenda shuleni, mimi niliona wasiwasi sana, hivyo mimi na makada wengine tulikwenda kuwahamasisha hao waende shule. Nakumbuka nilipomwuliza mtoto mmoja wa darasa la tatu, mbona hakwenda shule, alinijibu kuwa baba yake hakumruhusu, halafu nikamwuliza unapendelea wilaya ya Tashkurgan au kijiji cha Miskong? Akasema anapenda zaidi Tashkurgan, nilipomuuliza unapenda kitu gani cha Tashkurgan? Alisema shule ya huko ni nzuri."

    Bw. Guo Yukun anasema, alilia baada ya kusikia maneno ya mtoto huyo. Baba mzazi wa mtoto huyo alisema mtoto hana haki ya kutoa sauti, lakini Bw. Guo Yukun alimwambia, ingawa mtoto ana umri mdogo, lakini maneno aliyosema ni ya kweli zaidi. Unataka mtoto wako akiba tu mlimani kuchunga kondoo kama wewe ulivyo? Hatimaye watoto wote 18 waliruhusiwa kwenda shule, lakini unajua, iliwachukua muda wa siku 7 kufika shuleni.

    Shule hiyo ya bweni si kubwa, na ina wanafunzi 84 wanaosoma darasa la kwanza, pili na la tatu, na vilevile kuna walimu na wafanyakazi 15. Hali ya shuleni hapo ni ya duni, na milima na mito inawazuia wanafunzi hao kutoka nje, vilevile wanakabiliwa na ukosefu wa umeme na maisha magumu, na hawawezi kurudi nyumbani wanapokuwa shuleni kwa nusu mwaka, hivyo walimu na wanafunzi wana pilikapilika kila siku.

    Mbali na kufundisha, kila siku walimu wa shule hiyo pia wanawahudumia wanafunzi hao kwa maisha yao. Wanapoulizwa wana matumaini gani katika siku za baadaye, wanafunzi wengi hawajui kujibu, kwani kimsingi wamezoea maisha ya wazazi wao na mababu zao, kwamba wanapofikia umri wa miaka 12, wanafanya shughuli za ufugaji na kilimo, na wanapotimia miaka 20, wanafunga ndoa.

    Wang Ximei ni mwalimu katika shule hiyo. Watu wanamsifu kuwa ni mwalimu mzuri anayefundisha katika sehemu zenye hali duni ya kiuchumi nchini China. Baada ya kupata shahada ya uzamili ya masuala ya uongozi wa biashara MBA katika Chuo Kikuu cha Beijing, Wang alipata ajira katika kampuni ya uuzaji wa nyumba mjini Shenzhen, Guangdong. Mwaka 2011, Mei, Wang Ximei alijiuzulu na kuwa mwalimu wa shule ya msingi ya bweni katika tarafa ya Maryang, wilayani Tashkurgan Tajik. Anapozunguzia uamuzi huu, Wang anasema,

    "Wanafunzi wenzangu wamefunga ndoa na wamekuwa na watoto, hivyo hawawezi kuondoka nyumbani, lakini mimi bado sijaolewa, hivyo nina nafasi, vilevile nataka kuangalia mambo ya nje. Nimekuja hapa na mama yangu, ananisaidia kupika na kufua. Mtu wa kwanza anayejitolea niliyepata ni mama yangu."

    Hivi sasa wanafunzi wa shule hiyo wana matumaini mbalimbali, kwamba wanatarajia kuna njia inayounganisha tarafa hiyo na sehemu nyingine, ambapo watu wanaweza kutumia simu, na wanapozungumzia ndoto yao, baadhi yao wanasema,"Natarajia kusoma mjini Beijing, baada ya kukua, ningependa kuwa mwalimu wa uchoraji." "natarajia kusoma katika miji ya mingine nje ya hapa, nitasoma kwa bidii na kujipatia mafanikio ili wenzangu wa kabila la Watajik waone fahari, na kuwawezesha watu wa dunia nzima waone kuwa sisi Watajik ni hodari wa kuimba na kucheza dansi.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako