• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Mkurugenzi Jin Zhongyi anayetumia micro-blog

    (GMT+08:00) 2012-04-09 14:05:21

    Kama zilivyo nchi nyingine duniani, China nayo imeingia katika matumizi ya mtandao wa jamii. Utafiti uliofanyika hapa China unaonesha kuwa, hadi kufikia mwishoni mwa mwaka jana, idadi ya watumiaji waliosajiliwa wa micro-blog imefikia milioni 400. Ikiwa moja kati ya njia za mawasiliano ya umma na chombo cha habari chenye ushawishi, nguvu kubwa ya micro-blog imetambulika sana, hivyo hata serikali zinatumia micro-blog kukusanya maoni ya umma.

    Micro-blog inafanana na baraza kwenye mtandao wa internet na inawawezesha watumiaji wasome ujumbe na kuwafuatilia wengine, hii inaweza kuifanya habari iwafikie watu wengi na kwa mbali zaidi.

    Kwa mfano, kama mtu mmoja akituma ujumbe, wafuatiliaji wake wanaupata kwa wakati mmoja, na wanaweza kuutuma kwa mwingine. Ujumbe huo pia unaweza kuonekana katika microblog zao, na wakati huohuo, wafuatiliaji wao pia wanaweza kuuona kwa wakati mmoja. Hivyo ni rahisi sana kwa ujumbe huo kufika mbali katika muda mfupi.

    Jin Zhongyi, ana umri wa miaka 50, naye ni mkurugenzi wa idara ya sheria mjini Haining, mkoani Zhejiang, kusini mashariki mwa China. Yeye ni mtumiaji wa microblog, na idadi ya wafuatiliaji wake katika microblog imefikia laki 7.3.

    Mwanzoni mwa mwaka 2012, mkurugenzi huyo alichaguliwa kuwa mmoja kati ya maofisa 20 wa China wenye athari kubwa zaidi kwenye mtandao wa jamii, na baadaye ofisi 12 za sheria zilizo chini ya idara ya sheria mjini Haining zilianza rasmi matumizi ya microblog.

    Bw. Jin Zhongyi anasema microblog ni chombo kinachotumiwa na raia wa kawaida kutoa maoni yao, na kusimamia utendaji wa serikali, vilevile wanalinda haki yao. Microblog ni chombo chenye gharama ndogo na ufanisi mkubwa katika kufanya mawasiliano na kufuatilia mambo ya siasa. Bw. Jin Zhongyi anasema,

    "serikali inapaswa kutenda kazi kwa uwazi. Kutuma ujumbe kwa kupitia microblog kunawawezesha raia kushiriki katika kazi ya serikali, na wanaweza kusimamia kazi za serikali na kutoa maoni yao."

    Mkurugenzi huyo anapokea kirahisi mambo ya kisasa, kwani muda wote anatembea na kompyuta ndogo (laptop), ipad, simu ya mkononi aina ya iphone na kamera.

    Awali, Bw. Jin alitumia microblogging kwa ajili ya kusoma habari na kutoa maoni yake, baadaye aliwahamasisha watu wengine kufungua microblogging, na sasa anaziunganisha blogu hizo na kazi zake za kila siku. Akiwa mwanasheria, Jin anatumia microblog kutoa elimu ya sheria.

    Siku moja ya mwaka jana, Bw. Jin alisoma habari katika microblog iliyohusu ajali kubwa ya barabarani iliyosababishwa na gari moja kugonga mti barabarani kutokana na mwendo mkali, na dereva alikuwa hatarini. Bw. Jin alijibu wakati huohuo kwa kupitia microblog yake kuwa "marekebisho mapya ya sheria ya makosa ya jinai yanasema kuendesha gari kwa kasi ni kukiuka sheria, na watu wanaoendesha gari baada ya kunywa pombe au kushindana kwa kuendesha magari barabarani watakamatwa na kulipa faini."

    Bw. Jin Zhongyi anaona kuwa, kupitia microblog, idara za serikali na maofisa wanaweza kusikiliza maoni ya wananchi ili kurekebisha kazi zao. Anasema,

    "tunapopanga na kusimamia kazi, tunafuatilia sana maoni ya watu, na maoni yanayopinga yanaweza kutusaidia kurekebisha kwa wakati mipango yetu ya kazi, hii inalingana na maoni ya raia."

    Hatua ya Jin ya kufungua microblog na kuitumia katika kazi ya sheria na kujenga jukwaa la mawasiliano na watu inasifiwa na kufuatiliwa na viongozi wa ngazi ya juu. Naibu mkuu wa idara ya sheria mkoani Zhengjiang Lin Danjun anasema microblog inaweza kuongeza imani ya watu kwa serikali yao na kuongeza ushawishi wa idara ya sheria katika jamii. Anasema,

    "idara za serikali zinazofungua microblog rasmi zinaongezeka siku hadi siku, na zinawasiliana na wanamtandao na kufuatilia maoni ya watu, hili ni jaribio zuri katika kuboresha sifa ya serikali."

    Kushiriki mambo ya siasa kupitia mtandao wa jamii kunaonesha moyo wa kutetea demokrasia walio nao watu wa kawaida , pia ni njia mpya ya kuifanya kazi ya kisiasa itendeke kwa uwazi. Lakini wataalamu wanawakumbusha maofisa kuwa, ni lazima kudumisha mawasililano na umma kwa kupitia njia ya microblog, kusikiliza maoni na mapendekezo ya watu ili kuboresha kazi za utawala. Tunatarajia kuwa idara za serikali, maofisa na raia wanaweza kuwasiliana vizuri zaidi.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako