• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Maputo-Sudan yamtaka rais wa Msumbiji asuluhishe mgogoro kati ya Sudan na Sudan Kusini

    (GMT+08:00) 2012-04-20 10:36:16

    Waziri wa mambo ya nje wa Sudan Bw. Ali Karti tarehe 19 huko Maputo alisema, serikali ya Sudan inamtaka rais Armando Guebuza wa Msumbiji asuluhishe moja kwa moja au kufanya usuluhisho pamoja na Umoja wa Afrika ili kutafuta ufumbuzi wenye ufanisi, na kuzuia mgogoro kati ya Sudan na Sudan Kusini usitokee tena. Baada ya kukutana na rais Guebuza, Bw. Karti aliwaambia waandishi wa habari kuwa, alimkabidhi rais Guebuza barua kutoka kwa rais Omar al-Bashir wa Sudan, na kufahamisha mambo yaliyotokea hivi karibuni nchini Sudan. Bw. Karti alisisitiza kuwa serikali ya Sudan inataka kutafuta njia ya kuepusha mapambano kati yake na Sudan Kusini. Anaona kuwa Msumbiji ina uhusiano mzuri na Sudan, hivyo inaweza kutoa mchango katika kufanya mgogoro kati ya Sudan na Sudan Kusini usipambe moto.

    Bw. Karti alisema maendeleo ya hali ya sasa yamefanya Sudan na Sudan Kusini zisiweze kufikia makubaliano kuhusu kazi ya kuweka mpaka na kunufaika kwa pamoja mapato ya mafuta, na kuna uwezekano kuwa mapambano kati ya nchi hizo mbili yatalipuka. Lakini alisisitiza kuwa serikali ya Sudan inaamini kuwa kutimiza amani ni chaguo zuri kabisa kwa Sudan na Sudan Kusini.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako