• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Barua 0529

    (GMT+08:00) 2012-06-06 16:20:16
    Barua kutoka kwa msikilizaja wetu Namasaka S. Kelvin wa S.L.P 165 Bungoma Kenya anasema ama kwa hakika Idhaa ya Kiswahili ya Redio China kimataifa mnag'aa kama mbalamwezi, mnatarjiba isiyopimika kwenye mizani na kamwe hakuna Idhaa yoyote inayotuunganisha kanda hii ya Afrika Mashariki kama CRI, kwani imesimama kidete kwa miaka 50 ya utangazaji bora, hizi kweli ni juhudi za mchwa.

    Kwa kweli mimi kama mwanafunzi wa shule ya upili Bungoma ninawapa hongera za dhati kwa kujiamini katika upeperushaji maridhawa wa matangazo yenu shukrani zangu za dhati pia zimuendee mkuu wa Idhaa ya Kiswahili kwa kutuunganisha kama jamii moja na kuondoa utengano wa kitabaka, kifamilia, kijinsia na kutuleta pamoja kwani umoja ni nguvu na utengano ni udhaifu. Ama kwa kweli CRI ni redio yenye ukakamavu, umahiri, tajriba ushindi na yenye kuongoza kwenye safu nyingi. Nani kama redio hii. Ahsante sana.

    Tunakushukuru kwa dhati msikilizaji wetu Namasaka S. Kelvin kwa barua yako, kwakweli jitihada zote tunazofanya ni kwasababu ya kutaka kuwaridhisha wasikilizaji wetu wote kila pembe ya dunia, na tunawaahidi kuongeza juhudi zaidi katika kuwaletea vipindi bora na maridhawa kabisa ahsante sana.

    Na sasa ni maoni tuliyotumiwa na wasikilizaji wetu kupitia mtandao wa internate na kwanza ni Bw. Choma wa Choma baruapepe yake ni chomawachoma@yahoo.com S.L.P 108 Mpanda Tanzania anasema saduku la barua kwa nini hamsomi barua zagu? Kila siku ni wegine tu wanaosomewa, kwani mimi pia ni mwanachama wa CRI. Kila siku ya jumane nawafatilia. lakini, hamsomi barua zangu. Ili usomewe, unatakiwa ufanyaje. Kama mkiipata barua yagu, nawaomba mnitumiye, vitabu na kaleda. ili watoto wagu wajisomee, mimi kila siku watoto wananibana maswali vitabu vikowapi? baba kumbe na wazee ni waongo. jamani nawaomba lawama ni zitowe kwa watoto

    Kwanza tunakushukuru sana msikilizaji wetu Choma wa Choma kwa barua yako fupi ya malalamiko, kuhusu vitabu tutakutumia ili kukuondolea lawama kwa watoto wako, lakini suala la kutosoma barua si sahihi kwani hatujapokea barua zako kwa muda mrefu sasa, hivyo unapotuma barua hakikisha unatumia anuani sahihi, ahsante sana.

    Naye Yohana Marwa baruapepe yake ni marwa.yohana@yahoo.com anasema kipindi cha leo cha cheche zetu kimenivutia sana baada ya kumzungumzia mwanamziki maarufu OLIVA NGOMA ambae ni raia wa Gabon. Kiukweli mwanamziki huyo ni maarufu katika ulimwengu wa mziki. Mimi kitu ambacho nimegundua ni kuwa wanamziki wengi ambao hatukonao lakini tutazidi kuwakumbuka kwa mziki wao ambao waliucheza kabla ya kutangulia mbele ya haki kumbe, kama ni hivyo basi hatuna budi kuwaombea dua zetu kwa MUNGU ili roho zao zipumzike kwa AMANI. Hakika kipindi hiki kinatufahamisha mengi kuhusiana na wanamziki mbalimbali ambao ni wakongwe katika nyanja ya mziki na ambao walitamba miaka ya nyuma na bado hata leo nyimbo zao zinazidi kuvuma katika Ulimwengu wa mziki, nawapongeza sana muandaaji wa kipindi kizima cha cheche zetu kikirushwa hewani na idhaa ya kiswahili ya Radio China Kimataifa.

    Shukran nyingi sana Bwana Yohana Marwa kwa barua yako, salamu tumezifikisha kwa DJ Moss na tunakuomba uendelee kusikiliza zaidi vipindi vyetu, ahsante sana.

    Na maoni ya mwisho yanatoka kwa Okong'o Magaigwa wa Kemogemba Club S.L.P 71 Tarime ametumia sanduku la baruapepe la Yohana Marwa marwa.yohana@yahoo.com akisema wafanyakazi wa CRI nimesikiliza matango ya jumatatu ya tarehe 23/04/2012 kipindi cha sauti ya wanawake kuhusu kutokuwepo kwa uwiano kati ya idadi ya wanaume na wanawake nchini China kwa kweli nimevutiwa na kipindi hicho sana. Lakini vilevile nimesikitishwa na kile kinachosemekana kutoa mimba kwa wanawake wa kichina kwa kigezo kwamba watajifungua mtoto wa kike jambo ambalo ni hatia hata mbele ya MWENYEZI MUNGU.

    Na labda ningependa kufahamu jambo moja kuwa watu kama hao pale wanapobainika je, wanachukuliwa hatua gani na Serikali dhidi ya vitendo hivyo. Matangazo ni mazuri sana kwa hiyo nawaombea afya njema ili mwendelee kutupatia matangazo ya uhakika kwa sababu kile kinachotolewa na idhaa hii kinaendana na mahitaji yetu sisi wote. Baada ya kusema hayo naomba kusema akhasanteni sana idhaa ya kiswahili ya CRI kwa jinsi mnavyowajali wasikilizaji wenu popote pale walipo duniani kwani hamtumii lugha moja bali mnatumia lugha nyingi kuona kuwa matangazo yenu yanasambaa kama mawingu ya mvua na kutuwa popote yapendavyo ndivyo ninavyoweza kuilinganisha CRI Kutokana uimara wa uongozi wa CRI.

    CRI itazidi kuimarika siku hadi kutokana na kuwa inaendana na mahitaji ya wakati uliopo na hata wakati ujao kwani idhaa hii haipigi hatua moja mbele bali ni zaidi ya hatua elfu mbele zaidi, hivyo basi baada ya kugunduwa utamu wake ndo maana nikaamuwa kuwa msikilizaji hai wa idhaa ya kiswahili ya Radio China Kimataifa japokuwa nina siku nyingi bila kuwaandikia baruwa ila sikosi kutegea sikio matangazo ya CRI pale yanapokuwa hewani, basi naomba nisiwekwe kapuni, mimi ni hai katika idhaa yetu hii ya kiswahili ya CRI. Vilevile nilifurahia kipindi cha hivi karibuni kilichokuwa kikizungumzia Waafrika wanaoishi katika mji wa Guangzhou, hakika nilitamani na mimi siku moja nijikute katika mji huo na niweze kujionea kile kinachoendelea au kinacho fanywa na waafrika wenzangu huko. Mwisho nawatakia kazi njema na MUNGU awabariki sana akhasanteni sana.

    Shukrani za dhati msikilzaji wetu Okong'o Magaigwa kwa barua yako ya maoni kupitia kwenye mtandao wa internate, kwakweli kuhusu wanawake wanaotoa mimba kwa kuhofia kuzaa watoto wa kike, hatua kali zinachukuliwa, ikiwemo kupiga marufuku zahanati zinazofanya vitendo hivyo, pia serikali inahamasisha familia zinazozaa mtoto mmoja wa kike kwa kuwalipia masomo yao. Ahsante sana.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako