• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Rais wa Afrika Kusini afanya mabadiliko kwenye baraza la mawaziri

    (GMT+08:00) 2012-06-13 10:14:50

    Rais wa Afrika Kusini Jacob Zuma amefanya mabadiliko kwenye baraza la mawaziri ili kuimarisha mamlaka ya baraza hilo. Katika mabadiliko hayo yaliyofanywa jumanne mchana hakuna waziri yeyote aliyeondolewa madarakani, huku nafasi kadhaa zikiwa zimejazwa na wafuasi muhimu wa Zuma.

    Waziri wa ulinzi na wanajeshi wastaafu Lindiwe Sisulu amehamishwa katika idara ya huduma za jamii na uongozi, akichukua nafasi ya marehemu Roy Padayachee. Hatua hiyo ya kubadilishiwa kwenye wizara hiyo inachukuliwa kama ni kushushwa cheo, na inatokana na kuonesha huruma kwa aliyekuwa mwenyekiti wa umoja wa vijana wa ANC Julius Malema ambaye amefukuzwa kwenye nafasi hiyo, vilevile kulipuuza bunge kwa kukataa kujibu maswali bungeni.

    Mawaziri wengine waliobadilishwa ni pamoja na Novise Mapisa Ngakula ambaye amepelekwa wizara ya ulinzi na wanajeshi wastaafu, na Ben Martin atachukuwa nafasi ya Sibusiso Ndebele na kuwa waziri wa usafiri.

    Haya ni mabadiliko ya tatu tangu Zuma achaguliwe rais wa Afrika Kusini mwaka 2009.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako