Rais Hu Jintao wa China alikuwa na mazungumzo na rais Barack Obama wa Marekani, walipokuwa Los Cabos, Mexico kuhudhuria mkutano wa kundi la nchi 20. Kwenye mkutano wa jana marais hao walibadilishana maoni kuhusu uhusiano kati ya China na Marekani, kufufua uchumi wa dunia na masuala makubwa ya kikanda na kimataifa yanayofuatiliwa na pande hizo mbili. Hii ni mara ya 12 kwa marais hao kukutana tangu rais Barack Obama aingine madarakani.
© China Radio International.CRI. All Rights Reserved. 16A Shijingshan Road, Beijing, China. 100040 |