• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Misri yapunguza vizuizi kwenda Gaza kupitia forodha ya Rafah baada ya Bw Morsi kuwa rais

    (GMT+08:00) 2012-06-28 09:57:34

    Toka Rais mpya wa Misri Bw Mohamed Morsi achaguliwe kuwa rais vizuizi katika forodha ya Rafah vimepunguzwa. Maofisa wa Gaza wamesema zaidi ya watu 1000 wanavuka kila siku katika forodha hiyo tangu Bw Morsi alipotangazwa kuwa mshindi. Wengi wa watu wanaovuka kwenda Misri ni wanafunzi, wagonjwa, wafanyabiashara na wale wanaokwenda kuwatembelea jamaa zao. Mkurugenzi wa forodha wa Hamas Bw Mohamed Abu Sabha amesema katika siku mbili zilizopita wagaza wengi waliruhusiwa kuingia Misri, na Misri imeahidi kuwa itapunguza zaidi vizuizi vya kusafiri. Msemaji wa wizara ya mambo ya ndani ya Hamas amesema wizara yake ilisimamisha uandikishaji wa watu wanaotaka kwenda Misri kwa kuwa walikuwa wanazidi kikomo cha watu 500 kwa siku. Miezi mitatu tangu Bw Mubarak aondolewe madarakani Misri ilipunguza vizuizi na kuamua kufungua forodha kwa siku 6 kwa wiki badala ya siku 5.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako