• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Maandalizi ya michezo ya Olimpiki ya London yakaribia kumalizika

    (GMT+08:00) 2012-07-16 10:15:33

    Kazi ya maandalizi inakaribia kumalizika siku 12 tu kabla ya ufunguzi wa michezo ya Olimpiki ya London, huku wanariadha na maofisa kutoka nchi na sehemu mbalimbali duniani wakianza kuwasili London leo.

    Wenyeji wanakabiliwa na changamoto kubwa katika mambo ya mawasiliano na usalama. Kuna wasiwasi kwamba, mabasi na treni huenda zitashindwa kutokana na msogamano mkubwa wa watu.

    Hata hivyo Mark Evers, mkurugenzi anayeshughulikia mambo ya mawasiliano kwa ajili ya michezo ya Olimpiki amesema ana imani kubwa.

    "Tuna imani. Kwani wakazi wa London ni watu waliozoea harakati kubwa. Hata hivyo safari hii tunakabiliwa na changamoto ambazo haziwahi kutokea, kwa hiyo ni muhimu kwa wakazi wa London kuweka mpango kabla ili kuepuka sehemu zinazoweza kuwa na msomgamano."

    Wakati huo huo Victoria Bacon, ambaye ni mkuu wa shirikisho la mashirika ya utalii ya Uingereza, ameeleza matarajio kwamba, michezo ya Olimpiki itawavutia watalii wengi.

    "Michezo ya Olimpiki ni tukio kubwa katika maisha ya watu wanaokuja kuishuhudia. Naona itawavutia watu wengi sana."

    Makadirio yanaonesha kuwa, karibu watu laki 5 kutoka sehemu mbalimbali duniani wanatarajiwa kwenda London wakati wa michezo ya Olimpiki itakayofanyika kuanzia Julai hadi Agosti.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako