• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Nchi za maziwa makubwa zaamua kujenga kikosi cha pamoja cha kukabiliana na mgogoro wa mashariki mwa DRC

    (GMT+08:00) 2012-07-16 10:55:08

    Mkutano wa wakuu wa nchi za maziwa makubwa ICGLR jana umesaini azimio la kuanzisha kikosi cha pamoja kitakachoimarisha usalama wa mpaka kati ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo na Rwanda.

    Akizungumza na shirika la habari la Xinhua, China katibu mtendaji wa umoja huo Bw. Ntumba Luaba amesema, ukubwa wa kikosi hicho bado haujaamuliwa, lakini lengo lake ni kukabiliana na makundi ya waasi likiwemo kundi la M23 lililoko jimbo la Kivu kaskazini.

    Ameongeza kuwa, mkutano utakaowashirikisha wataalamu wa kijeshi na mawaziri wa ulinzi wa nchi za ICGLR utafanyika mwishoni mwa Julai, na utalenga kutafuta njia za kufanikisha kazi za kikosi hicho kama vile ukubwa wake, mahitaji yake na maeneo yake ya kazi.

    Marais wa Rwanda, DRC, Tanzania, Uganda na Afrika ya Kati walishiriki kwenye mkutano huo mkuu.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako