• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Eldoret chimbuko la mabingwa wa wariadha duniani.

    (GMT+08:00) 2012-07-24 19:54:16

    Wanariadha walikimbia mapema asubuhi katika kambi ya riadha ya Iteen jijini Eldoret wakati wa mazoezi ya kujitayarisha kwenye mashindano ya olimpiki yatakayoandaliwa jijini London Uingereza mwaka huu wa 2012.

    Iten ni kambi ya wanariadha iliopo jijini Eldoret mji uliopata umaarufu mkubwa sana nchini Kenya na dunia nzima kwa kuwa chimbuko la wanariadha maarufu sana wa Kenya wanaotambuliwa ulimwenguni.

    Miongoni mwao ni Kipchoge Keino na Henry Rono waliokuwa wanariadha wa kwanza kushinda mbio za marathon za dunia zaidi ya miaka 20 iliopita.

    Katika historia ,Eldoret ni mji uliowahi kuzalisha wanariadha wa kimataifa wengi zaidi ya mji wowote ulimwenguni,na hapa nchini Kenya mji huu umechangia kuchipuza kwa asilimia 99 ya wanariadha wa taifa hili.

    Na hapo sasa linazuka swala la Je ni jambo gani linaloufanya mji huu kuwa makao makuu ya mabingwa wa riadha duniani?

    Katika ziara yetu mjini humu tulitembelea kambi ya Iteen,sehemu wanapopiga kambi na kufanya mazoezi wanariadha wengi wa Kenya pamoja na hata wale wa kimatiafa kutoka nchi mbali mbali.

    Baada ya kukaribishwa katika kambi hii ,tulikutana na Edwin Kiprotich mmoja wa wakaazi wa hapa ambae pia mwanariadha,alitueleza kuwa idadi kubwa ya wakaazi wa Eldoret ni wakalenjin,na kwa ufahamu wake wakalenjin wamebarikiwa sana na kipawa cha kukimbia ,hivyo wameugeuza mji huo kuwa makao ya ushindi wa riadha kutoka enzi za wazee wao hadi leo kutokana na vipawa vya kukimbia.

    Kalenjin wameshinda asilimia 70 ya medali za mashindano ya olimpiki katika mbio za masafa marefu tangu mwaka 1930.Wanariadha wa Kalenjin wameshinda nishani 26 nane za dhahabu kwenye mashindano ya olimpiki tangu mwaka 1980.

    Wakaazi wngi wa Iten wanaamini kuwa kutokana na ufanisi uliopatikana na wanariadha wa zamani walioshinda mashindano ya kimataifa wao pia wana nafasi ya kushinda.

    Hivyo idadi kubwa ya vijana hujiingiza kwenye riadha ili nao wapate nafasi ya kushinda japo sio wote wanaofanikiwa.

    Miongoni mwa wachache tulioongea nao wanatueleza kuwa mafanikio yao makubwa na hamu yao kuu ya kushiriki kwenye riadha ni kukuza vipaji vyao.

    Baadhi yao wanaelezea kuwa riadha katika eneo hilo imekuwa ni kama maisha yao hivyo mafanikio yao hutokana na juhudi wanazozifanya.

    Aidha kwa wingine riadha sasa imekuwa njia moja ya kujitafutia pesa ya kubadilisha maisha yao pamoja na kujipatia sifa tele ulimwengu mzima, jambo ambalo limepelekea wazazi wa eneo hilo kuwahimiza sana watoto wao kushiriki kwenye riadha haya ni kwa mujibu wa maoni ya James Kemboi

    Sababu nyingine muafaka ya kijeografia inayoipatia Iten uwezo wa kutoa wakimbiaji bora duniani ni sehemu ya ardhi yake.Eneo hili liko kwenye bonde la ufa llinalopatikana katika usawa wa futi 7875 kutoka baharini.

    Umbali huu wa ardhi yao yenye milima na mabonde bila shaka inaotoa nafasi nzuri ya mazoezi magumu yanayowafanya wanariadha kukomaa kimwili na kuwa nguvu nyingi kama anavosimulia Alex Jepkosgei.anasema wakaazi wa wapa hupanda milima na kuishuka kulisha wanyama wao ambayo ni kama njia moja ya mazoezi.

     

    Kwa wakati huu zaidi ya wanariadha 100 kutoka nchi za nje wanaendelea na mazoezi yao katika kambi ya Iten,wao huamini kuwa washindi wote hutoka Iten na wao pia watakuwa washindi wakifanya mazoezi kwenye kambi hiyo.

    Mabingwa wa dunia kama vile Wilson Kipketer bingwa wa dunia mita 800 raia wa Denmark,Sally Barsosio aliekuwa bingwa wa olimpiki mita 1500 na Bernad Lagat kutoka Marekani waliwahi wakati mmoja kufanya mazoezi katika kambi ya Iten.

    Miongoni mwa sababu nyingine zinazokuza vipaji vya wanariadha hapa Eldoret ni kuwa ,wakaazi wa hapa wengi hawakuzoea kutumia magari kama usafiri wao ,hivyo wakiwa wadogo wanafunzi hukimbia kilomita nyingi sana kuenda shule hali inayowaanzisha mazoezi mapema.

    Aidha wakaazi wa hapa pia wanakula vyakula vizuri bila ya kemikali zinazopunguza nguvu za mwili na kusababisha maradhi.

    Alex Jepkogei ni kocha wa riadha mwanariadha tuliemkuta kwenye mazoezi, yeye anajiandaa kwa mbio za marathon za mwaka ujao ,anatusimulia kwa kina kuwa mbali na kipaji cha kukimbia walichopewa wakalenjin,bidii imekuwa chanzo kikuu cha mafanikio kwa wanariadha kwani mbali na kushinda medali na kupata sifa za ulimwengu mzima ,wao pia hutumia mbio hizo kama kipato chao cha kibiashara kwani hupokea malipo ya pesa nyingi wanaposhinda mashindano ya kimatiafa

    Takwimu zinaonyesha wazi kuwa wanariadha wa Kalenjin hususan kutoka kambi ya kambi ya Iten ya Eldoret ni kitovu cha mabingwa wa riadha duniani.Kwa jumla Kenya imeshinda nishani 28 za mashindano ya Marathon katika mashindano 30 walioshiriki duniani.

    Aidha wanariadha wa Kenya wamenyakuwa jumla ya nishani 54 kwenye mashindano ya olimpiki ,17 dhahabu ,24 fedha na 20 shaba.

    Kutokana umaarufu wa kambi hii wanariadha hata kutoka China sasa wamekuja Iten kufanya mazoezi ya riadha wakiwa na matumaini kuwa pia wao wanaweza kuwa washindi kutokana maandalizi kabambe pamoja na bahati ya mji wa Eldoret kutoa washindi.

    Kwa kweli chanda chema huvishwa pete na wanariadha wa Eldoret ni mafahali wa kupigiwa mfano duniani.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako